Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta, akimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Mathew Luhanga.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta, akisaini kitabu cha wageni kabla ya kuanza mahafali ya 16 kampasi ya Dar es Salaam.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro (kushoto) akiwa na Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi.
Brass Band ikiongoza maandamano.
Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali.
Maandamano ya kitaaluma kuelekea sehemu ya mahafali.
Maandamano ya kitaaluma kuelekea sehemu ya mahafali.
Mlau, Prof. Binamungu akiongoza maandamano kuelekea sehemu ya mahafali.
Meza Kuu.
Wanataaluma.
Wahitimu.
Mlau, Prof. Binamungu akitoa nasaha zake.
Wahitimu wa Shahada ya Umahiri ya Sayansi katika Menejimenti ya Rasilimali Watu.
Baadhi ya wahitimu wa shahada mbalimbali wakiwa katika mahafali hayo.
Mwenyekiti wa Baraza la Chuo, Prof. Mathew Luhanga, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. Lughano Kusiluka, akitoa hotuba yake wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu Barnabas Samatta.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi (kushoto) akiwa na Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro, wakifuatilia kwa makini mahafali hayo.
Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kampasi ya Dar es Salaam, Dk. Lucy Massoi, akiwatambua wanachuo na wahadhiri waliofanya vizuri.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Gloria Mbigiri wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe Jaji mstaafu, Barnabas Samatta, akimkabidhi cheti mmoja wa wanachuo aliyefanya vizuri, Elihuruma Mabelya wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.
Baadhi ya wahitimu wa Shahada ya Umahiri ya Uongozi wa Biashara katika Menejimenti ya Biashara wakitunukiwa shahada zao na Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Jaji mstaafu, Barnabas Samatta (hayupo pichani), wakati wa mahafali ya 16 ya chuo hicho kampasi ya Dar es Salaam.
Mmoja wa wahitimu waliofanya vizuri.
Wahitimu.
Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taalum, Prof. Ganka Nyamsogoro.
NA MWANDISHI WETU
MAKAMU Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Lughano Kusiluka, amesema wahitimu 610 wa Shahada mbalimbli kutoka chuoni hapo wanauwezo wa kuongeza chachu kwenye uchumi wa viwanda kwa kuwa wamepata ujuzi bora.
Akizungumza jijini Dar es Salaam juzi wakati wa mahafali ya 16 ya Chuo Kikuu Mzumbe kampasi ya Dar es Salaam, Profesa Kusiluka alisema ubora wa elimu inayotolewa katika chuo hicho unachangia katika kuwaandaa wataalam mbalimbali kwenye sekta ya viwanda.
Alisema uongozi wa chuo chake unaunga mkono falsafa ya Rais John Magufuli ya kuwa na Tanzania ya Viwanda kwa kuhakikisha wahitimu wa Chuo Kikuu Mzumbe wanaweza kushindana kwenye soko la ajira za viwandani.
"Ubora wa elimu yetu unadhibitishwa na ongezeko la wanafunzi hapa chuoni kwetu... Tulianza hapa Dar es Saalam mwaka 2005 tukiwa na kozi mbili zilizokuwa na wanafunzi 156.
"....Leo idadi ya wadahiliwa na wahitimu imeongezeka, kutoka wahitimu 156 miaka 12 iliyopita hadi wahitimu 1,335 na hapa tulipo wahitimu ni 610 wa shahada mbalimbali kati yao wanawake ni 331 na wanaume ni 279," alisema Profesa Kusiluka.
No comments:
Post a Comment