HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

December 02, 2017

Mandozi kufungua kijiji cha michezo Misungwi

NA MWANDISHI WETU

KITUO cha Michezo cha Mandozi Sport Academy kinatarajia kufungua kijiji cha michezo Januari 3 mwaka 2018 kitakachokuwa Sumve wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Hayo yamesemwa na Meneja wa Kituo hicho Mohamed Ngaiza wakati akizungumza na Sayari kwa njia ya simu kutoka Mwanza.

Ngaiza alisema wamelazimika kufungua kijiji hicho ambacho kitaweza kuchukua watoto zaidi ya 20 kwa pamoja ili kuweza kukuza vipaji vya vijana ambao wanashiriki mchezo wa mpira nchini.

Alisema kwa sasa wanatarajia kijiji hicho kitachukua vijana hao 20 huku matarajio yakiwa ni kuhakikisha kuwa wanachukua vijana 50 wa rika mbalimbali kuanzia miaka 8 hadi 20.

“Mandozi Sports Academy ni kituo ambacho kimeanzishwa miaka mine iliyopota na matarajio yetu ni kuhakikisha kuwa vijana wenye vipaji vya mpira wanapata msingi mzuri na matunda yameshapatikana kwani tumewatoa Selemani Hamisi wa Ruvu Shooting na Pius Buswita wa Yanga,” alisema.

Meneja huyo alisema matarajio yao ni kuona kijiji hicho kutoa vijana ambao watakuwa na ujuzi mbalimbali ikiwemo kucheza mpira, kujifunza maisha ya ujasiriamali na kusoma.

Ngaiza alisema katika kuhakikisha vijana hao wanaishi katika misingi ya kisheria na nidhamu wanawapatia mikataba ya kisheria ili kuepuka ulaghai ambao umekuwa ukitokea mara kwa mara kwa wachezaji wao.

Aidha alisema wamefanya mawasiliano na wakala na vilabu mbalimbali ili kuhakikisha kuwa wanauza wachezaji wao kwa kufuata misingi na taratibu za kisheria.

“Tumewasiliana na Alex Kajumulo yupo Marekani, Rwanda tuna wakala, pia klabu ya Azama na Kagera Sukari tumekubaliana kushirikiana naamini siku moja Mandozi itakufanikiwa,” alisema. Alisema malengo makubwa ni kuuza wachezaji wankidhi sifa ili kuruhusu vijana wengine wenye vipaji kuingia kuonesha vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment

Pages