NA MWANDISHI WETU
BAADHI ya wastaafu wa iliyokuwa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), wamesema wameridhishwa na tamko la Rais John Magufuli la kwamba anazo taarifa kuwa Kampuni ya Simu za mkononi Aitel ni ya serikali.
Wafanyakazi hao waliyasema hayo kwa vile wanauhakika kabisa Kampuni hiyo ilitenganishwa na TTCL kutokana na masilahi binafsi kitendo kilichozua manung'uniko kutoka kwa wafanyakazi waliobaki TTCL kipindi hicho.
Wakizungumza na Habari Mseto, jijini leo, kwanyakati tofauti wafanyakazi hao, walisema wanamuomba Rais Magufuli, aendelee kuutafuta ukweli hadi kieleweke.
Walisema wamefikia hatua hiyo kwa vile kampuni hiyo ilianzishwa kutokana na fedha za iliyokuwa kampuni kongwe ya TTCL.
"Unajua kutenganishwa kapuni hiyo ya Airtel kulizua mgogoro mkubwa kati ya wafanyakazi wa TTCL na uongozi kikubwa tulikuwa tunadai fedha zetu," alisema mmoja wa wastaaafu hao, Seifu Mbwana.
Mbwana, alisema anachofanya rais ni sawa na kuungana na wafanyakazi wa kampuni ya TTCL ambao walipinga kitendo hicho cha kuporwa kampuni yao ambayo waliamini ingefanya vizuri kuliko kampuni yeyote ya simu za mkoni nchini.
Aisha Sangale, alisema walipinga kutenganishwa kampuni hiyo lakini baadhi ya viongozi wa serikali ambao wengine waliwahi kuwa kwenye bodi kipindi hicho kulazimisha kukamilika kwa mpango huo tena haraka.
"Nakumbuka baada ya mpango huo kukamilika ili tubidi wafanyakazi tudai kulipwa fedha kama fidia kwa asababu kampuni hiyo ya Airtel ilianzishwa na fedha za kampuni ya TTCL.
Hata hivyo, Aisha alisema jitihada zao za kudai malipo hayo ziligonga mwamba baada ya uongozi kutumia lugha za ulaghai kwamba wangelipwa.
"Sisi hatushangai na wala hatulioni jambo hili kama ni jipya bali tunasikitika kwamba wakati tunaipigania Airtel kipindi kile isitenganishwe serikali haikujali,"alisema Aisha.
Aidha, Aisha, alisema licha ya uongozi kipindi hicho kutumia ulaghai kwamba ungelipa wafanyakazi hao waliobaki TTCL baada ya kampuni hizo kutenganishwa kwa kuingiza mgao kwenye Akaunti ya kila mfanyakazi lakini yote hayo hayakufanyika hadi sasa.
No comments:
Post a Comment