HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 18, 2018

FAMILIA ILIYODHURUMIWA KIWANJA YAMUOMBA RAIS MAGUFULI KUWASAIDIA KUPATA HAKI YAO

 
Msemaji wa familia ya Marehemu Iddi Tosiri, Iddi Tosiri akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya kudhurumiwa kiwanja cha marehemu baba yako kilichopo mtaa wa Ukami Kariakoo jijini Dar es Salaam Januari 17, 2018.


Huyo ni Mtoto wa marehemu Iddi Tosiri, Maulid Tosiri.


NA JANETH JOVIN
FAMILIA ya marehemu Iddi Tosiri imemuomba Rais John Magufuli awasaidie kupata haki yao ya kupata kiwanja walichodhurumiwa.

Familia hiyo imedai kuwa wamedhurumiwa kiwanja cha marehemu baba yao chenye namba 11 block70-L 10270 kilichopo mtaa wa Ukami Kariakoo jijini Dar es Salaama.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Januari 17, 2018 Msemaji wa familia hiyo, Iddi Tosiri alisema marehemu baba yao alikuwa akifanya kazi kwa wakoloni na kupata fedha zilizomuwezesha kununua viwanja mbalimbali.

Alisema pamoja na viwanja vingi alivyonunua kipo kimoja ambacho alidhurumiwa na wakili wake aliyempatia kazi ya kubadilisha jina la hati ya kiwanja hicho alichopewa kwa umiliki wa miaka 99.

"Marehemu alimkabidhi wakili huyo hati hiyo mbele ya mashahidi na kiwanja hicho kilikuwa na nyumba ambayo baba yetu alinunua mwaka 1958,hata hivyo wakili huyo alibadili hati na kudanganya kuwa yeye ameomba kupewa kiwanja hicho kwani hakukuwa na kitu jambo ambalo si kweli.

Licha ya kudai haki yetu kwa muda mrefu kwa kupeleka vielelezo lakini tumekwama kutokana na mlalamikiwa kukingiwa kifua na baadhi ya watu serikalini, hivyo basi tunamuomba Rais mtetezi wa wanyonge aingilie kati na atusaidie katika hili,"alisema.

Naye Mtoto wa Marehemu, Maulid Tosiri alisema marehemu baba yake amefanya kazi kubwa na kuwa mstari wa mbele wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

No comments:

Post a Comment

Pages