WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amesema hajaridhishwa na ubora wa ujenzi wa kituo
cha forodha cha Sirari kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya.
Kufuatia
hali hiyo amemtaka Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) afike
ofisi ya Waziri Mkuu mjini Dodoma akiwa na mkandarasi aliyejenga kituo
hicho.
“Serikali
haiwezi kuvumilia ujenzi wa hovyo kiasi hiki, namtaka Kamishna wa TRA
aje ofisini kwangu Januari 25, 2018 pamoja na mkandarasi aliyejenga
kituo hiki akiwa na nyaraka zote za ujenzi wa jengo hilo.”
Ameyasema
hayo leo (Jumatano, Januari 17, 2018) mara baada ya kumaliza kukagua
kituo hicho kilichopo wilayani Tarime, akiwa katika ziara yake ya kikazi
mkoani Mara.
Waziri
Mkuu amesema hajaridhishwa na ujenzi huo kwa kuwa upo chini ya kiwango.
Kituo hicho kilianza kujengwa mwaka 2011 na kukamilika mwaka 2014.
Waziri
Mkuu amejionea mwenyewe kuta za jengo hilo zikiwa na nyufa nyingi
kuanzia ukutani hadi sakafuni na pia rangi za baadhi ya kuta zikiwa
zimebanduka.
Katika hatua nyingine,
Waziri Mkuu amewataka wananchi wa wilaya hiyo kufanya shughuli zao za
kiuchumi kwa kuzingatia sheria na wajiepusha na biashara za magendo.
Waziri
Mkuu amesema magendo yanaikosesha Serikali mapato, hivyo bidhaa yoyote
itakayokamatwa ikiingizwa nchini kwa njia za magendo itataifishwa pamoja
na chombo cha usafiri kilichotumika.
Pia Waziri
Mkuu ametembelea shule ya Sekondari ya Wasichana ya Borega, ambapo
amewasisiza wananchi wasimamie elimu ya watoto wa kike ili wafikie
malengo yao.
Amesema
Serikali imeweka sheria kali kwa yeyote atakayekatisha masomo kwa
watoto wa kike iwe kwa kumpa ujauzito au kumoa, adhabu yake ni kifungo
cha miaka 30 jela.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu amewataka wanafunzi hao wasome kwa bidii ili waweze
kutimiza ndoto zao na kamwe wasijihusishe katika mambo ambayo
hayahusiani na masomo.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 17, 2017.
No comments:
Post a Comment