HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 26, 2018

HALOTEL YASAIDIA UJENZI OFISI ZA WALIMU

Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Pham Dinh Quanakizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa Sh. Mill 50. zilizotolewa na Halotel kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402.
Mkurugenzi Mkurugenzi wa Kampuni ya Simu ya Halotel, Pham Dinh Quan (kushoto), akimkabidhi mfano wa hundi ya Sh. Mill. 50 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402. (Picha na Francis Dande).

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya simu za mkononi Halotel, imetoa sh. Milioni 50 kwa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ili kujenga ujenzi wa ofisi za walimu kwa shule 402.

Akizungumza jana katika hafla ya kukabidhi fedha hizo, Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Halotel, Le Van Dai, alisema kwamba mchango huo ni sehemu ya jitihada zinazofanywa na kampuni hiyo kusaidia na kuinua sekta ya elimu nchini.

“Tunatambua kwamba huduma bora ya elimu kwa wanafunzi na walimu ni moja ya msingi imara katika kukuza sekta hiyo, kwa kuzingatia hilo tumeamua kushirikiana na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutoa mchango wetu ili kufanikisha mradi wa ujenzi wa ofisi za walimu na kuboresha mazingira ya utendaji kazi kwa walimu na kurahisisha ufanisi wao,”alisema.

Aidha alisema kwamba kwasasa wametekeleza mtaji wa kuunganisha shule zaidi ya 400 nchi nzima na huduma ya intaneti ni ya kipekee ambayo inawanufaisha walimu na wanafunzi.

Alisema kwa kushirikiana na Nadki  ya teknolojia za habari na mawasiliano (CoICT) cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wameunda mfumo wa kujisomea kupitia mtandao wenye masomo ya sayansi na hisabati kwa kufuata mitaala inayokubalika.

No comments:

Post a Comment

Pages