*Asisitiza kwamba atakayebainika atashughulikiwa hapo
hapo
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amewataka watumishi wa umma nchini wasijihusishe na vitendo vya wizi, ufisadi
kwani Serikali haitosubiri kuwaundia tume za kuwachunguza bali itawashughulikia
hapo hapo.
Amesema Serikali haikotayari
kuwavumilia watumishi wanaojihusisha na wizi, ubadhilifu, rushwa na uzembe,
hivyo ni vema viongozi waliopewa dhamana wahakikishe wanatekeleza majukumu yao kwa
uadilifu.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo
jana jioni (Jumatatu, Januari 15, 2018) wakati akizungumza na watumishi wa
wilaya ya Musoma mkoani Mara akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya
kikazi ya siku sita mkoani hapa.
“Fedha zinazotolewa na
Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo zinalenga
kutatua kero za wananchi na si kuwanufaisha wachache wenye tamaa. Kama ni za
ujenzi wa zahanati ijengwe na atakayezitafuna Serikali haitosita kumchukulia
hatua.”
Waziri Mkuu asiwasisitiza watumishi
wa umma kufanya kazi kwa mujibu wa sharia kwa sababu vitendo vya wizi, uzembe vinachangia
kupunguza kasi ya kuwaletea maendelea maendeleo Watanzania.
Alisema lengo ni kuhakikisha
azma ya Serikali ya kuwaletea maendeleo wananchi hususan ni wale wa hali ya
chini inatimia, hivyo aliwaagiza viongozi wa halmashauri wakiwemo Madiwani
kusimamia vizuri miradi ya maendeleo.
Pia Waziri Mkuu aliwataka
wakuu wa idara na watendaji wengine wa halmashauri kuacha tabia ya kukaa
ofisini na dabala yake waende vijijini kwa ajili ya kuwafuata wananchi na kushirikiana
nao katika kutatua kero mbalimbali zinazowakabili.
Waziri Mkuu alisema watendaji
hao wanatakiwa waachane na tabia ya kuwasubiri wananchi wawapelekee malalamiko
yao kwa sababu baadhi yao hawana uwezo wa kufika katika ofisi zao.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMANNE, JANUARI 16, 2017.
No comments:
Post a Comment