Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandikwa, akitoa maelekezo kwa Mkandarasi Dott Service na
Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya Kyongdong Engineering
wanaojenga barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50 kwa kiwango cha
lami na kumtaka Mkandarasi huyo kukamilisha ujenzi wa barabara hiyo haraka. Imetolewa na Kitengo
cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Mbunge wa Jimbo la
Nanyamba mkoani Mtwara, Mheshimiwa Abdallah Chikota (Wa kwanza kulia),
akimuonesha Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa, (Wa pili kulia) sehemu
yenye mteremko mkali katika mlima wa Nameleche uliopo katika barabara ya
Mtwara-Mnivata-Tandahimba-Newala hadi Masasi yenye urefu wa KM 210 ambapo
magari husumbuka katika kipindi cha mvua kutokana na mteremko huo.
Naibu Waziri wa
Ujenzi, Elias Kwandikwa, akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mnivata mkoani
Mtwara alipofika hapo kukagua barabara ya Mtwara – Mnivata yenye urefu wa KM 50
inayojengwa kwa kiwango cha lami.
No comments:
Post a Comment