Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu)
Mhe.Jenista Mhagama akitoa tamko la Serikali leo mjini Dodoma kuhusu Kusitishwa
kwa Shughuli za Kampuni zinazotoa huduma ya Uwakala Binafsi wa Ajira baada ya
kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution
Company Ltd, Bravo Job Centre Agency na Competitive
Manpower International Ltd ambapo Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na
shughuli za Uwakala Binafsi wa
Ajira nchini, Januari 25, 2018.
Na Mwandishi Wetu
Na Mwandishi Wetu
Serikali yasitisha Shughuli
za Kampuni Tatu (3) za Wakala Binafsi wa Huduma za Ajira hapa Nchini kutokana
na kukiuka matakwa ya sheria ya Huduma za Ajira Na.9 ya mwaka 1999 na Kanuni
zake.
Akitoa tamko la Serikali
kuhusu Kusitishwa kwa Shughuli za Kampuni hizo Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.
Jenista Mhagama amesema kuwa Ofisi yake imekuwa ikipokea
malalamiko kutoka kwa wafanyakazi na wadau mbalimbali kuhusu utaratibu
unaotumiwa na baadhi ya Wakala Binafsi wa huduma za Ajira nchini.
Kampuni zilizofutiwa usajili
baada ya kukiuka sheria ni pamoja na Sasy Solution Company Ltd, Bravo Job Centre
Agency na Competitive Manpower International Ltd ambapo
Kampuni hizo haziruhusiwi kujihusisha na shughuli za Uwakala Binafsi wa Ajira nchini.
Akifafanua Mhe. Mhagama
amesema kuwa uchunguzi umebaini
ukiukwaji wa taratibu za usajili ambapo baadhi ya Mawakala wamekuwa wakitumia
nyaraka zilizopatikana kwa njia isivyo halali katika kujipatia leseni za
uwakala hali iliyowawezesha kukwepa kodi na kujipatia faida.
Aliongeza kuwa ukiukwaji wa
taratibu za kisheria umeleta athari mbalimbali kwa wafanyakazi hasa kwa wale
wanaoenda kufanya kazi Mataifa ya Nje ambapo wafanyakazi hao wamekuwa
wakifanyiwa vitendo vya ubaguzi na unyanyasaji katika ajira, malipo ya
mishahara na stahiki mbalimbali.
Aidha, Mhe. Mhagama amesema
kuwa Ofisi ya Waziri Mkuu imesitisha mara moja shughuli za Mawakala Binafsi wa
huduma za Ajira zinazohusika na kuwatafutia kazi wafanyakazi nje ya nchi (cross border placement) hadi hapo
Serikali itakapoleta mfumo wa kusimamia jambo hili na kutoa taarifa kwa umma.
Vile Vile, Waziri Mhagama
amemwagiza Kamishna wa Kazi kuhakikisha kuwa ndani ya wiki mbili kuzifanyia
uhakiki Wakala zote zilizosajiliwa kuona kama wametimiza na kuzingatia Sheria
na Kanuni zinazosimamia Wakala Binafsi za Ajira, Pia aliiasa Timu ya wakaguzi
itakayoundwa na Wizara ikikiuka miiko ya ukaguzi na kuficha udhaifu wa mawakala
hao hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa Mujibu wa Sheria na Kanuni za Utumishi
wa Umma.
No comments:
Post a Comment