Makamu wa Rais (katikati) Samia Suluhu Hassan akipata maelezo juu ya
ujenzi wa ukuta wa Kigamboni kutoka kwa Mkurugenzi wa Kampuni ya Dezo
Civil Contractors Co. Ltd, Premji Pindoria (kushoto) kulia NIU Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Poul Makonda. (Picha na Janeth Jovin).
NA JANETH JOVIN
MAKAMU wa Rais Samia Suluhu Hassan amewataka watanzania
kuyatunza mazingira yanayowazunguka ili kuepukana na athari za
mabadiliko ya tabianchi.
Mama Samia amesema kama jamii haitaweza kufanya hivyo basi
hupo uwezekano mkubwa katika maeneo ya nchi hasa kwenye fukwe za Bahari
ardhi yake kumomonyoka.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati ziara ya
kikazi ya kukagua ujenzi wa ukuta katika fukwe ya Kigamboni na Ocean
Road, Samia alisema kwa sasa mazingira yameanza kuharibiwa nchini hivyo
ni muhimu kuchukua hatua ya kuzuia yale yote yanayosababisha uharibifu
huo.
Alisema ni lazima kila mtu kuwa rafiki wa mazingira kwa
kuacha kukata miti hovyo na kutochimba mchanga baharini na kwenye vyanzo
vya maji.
"Suala la mazingira ni letu sote na tukumbuke kuwa
unapoharibu mazingira lazima yatakuja kukuadhibu baadae hivyo niwaombe
wananchi wayatunze ili yatutunze na tuweze kukabiliana na mabadiliko ya
tabianchi, "alisema.
Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia Muungano na Mazingira, January Makamba alisema mradi
huo wa ukuta ni miongoni mwa miradi mbalimbali ya kukabiliana na athari
za mabadiliko ya tabianchi.
Alisema mradi huo ambao umekamilika kwa asilimia 93 utazuia
kubomoka kwa chuo cha Mwalimu Nyerere kilichopo Kigamboni jijini Dar es
Salaam.
"Nchi yetu inaufukwe wa bahari upatao Kilomita 1400, eneo
hili ni kubwa na athari zilizopo huko kutokana na watu kutotunza
mazingira ni kubwa mno hivyo ni muhimu kuendelea kupaza sauti na kukemea
uharibifu wa mazingira, " alisema.
Naye Meneja mradi huo Fred Manyika alisema urefu wa ukuta uliyojengwa kigamboni ni Mita 500 na wa Ocean Road ni mita 920.
No comments:
Post a Comment