*Ni wa ujenzi wa Makao Makuu ya
Halmashauri ya Wilaya ya Tarime
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemaliza mgogoro wa ujenzi wa makao makuu ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime
mkoani Mara ambao umedumu kwa miaka mitatu.
Ametoa uamuzi huo leo (Jumatano,
Januari 17, 2018) wakati akizungumza na watumishi na madiwani wa Halmashauri ya
Wilaya ya Tarime pamoja na Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Amesema amesitisha mpango huo wa
ujenzi wa makao makuu ya halmashauri hiyo kwa kuwa imepangwa kujenga katika eneo
ambalo lipo mbali na wananchi.
“Ninazo taarifa kuwa mnataka kujenga katika
eneo ambalo litaigharimu Serikali kutumia fedha nyingi kwa ajili ya fidia na
pia lipo mbali na makazi ya wananchi.”
Pia Waziri Mkuu amesema Serikali haiwezi
kuruhusu ujenzi huo ufanyike katika eneo ambalo ni mbali ya makazi ya wananchi
kwa kuwa watashindwa kufuata huduma.
Hata hivyo, Waziri Mkuu amesema
Serikali itapeleka wataalamu watakaofanya uchunguzi na bainisha eneo sahihi la
kujenga Halmashauri hiyo kwa kutumia ramani.
Wakati huohuo, Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma kutotamani fedha za
maendeleo zinazotolewa na Serikali ajili ya miradi ya maendeleo.
Amesisitiza kwamba wasipokuwa makini
na fedha hizo zitasababisha wachukuliwe hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na
kuondolewa kazini. ”Je mpo tayari kuchukuliwa hatua.?
Amesema Serikali inapeleka fedha
kwenye halmashauri kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maendeleo ya
wananchi na si kuwanufaisha watu binafsi.
Pia amewataka watumishi kuacha
kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wawe wabunifu na wajue halmashauri zao
zinahitaji nini ili kuweza kusonga mbele kimaendeleo.
Waziri Mkuu ambaye leo ameendelea na
ziara yake Mkoani Mara kwa kutembelea wilaya ya Tarime ambapo baada ya kuzungumza na watumishi
alikagua hopitali ya Tarime na kuweka jiwe la msingi katika kituo cha afya cha
Sirari.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU
JUMATANO, JANUARI 17, 2017.
No comments:
Post a Comment