HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

January 17, 2018

MKAZI WA DAR NA KIGOMA WAJISHINDIA KITITA CHA MILIONI 10 KILA MMOJA


Akizungumza na waandishi habari wakati wa kukabidhi mfano wa hundi hizo kwa washindi hao, mapema leo mbele ya Waandishi wa Habari (hawapo pichani), Mmoja wa Maofisa Habari wa Tatu Mzuka, Millard Ayo, alisema kuwa droo hiyo inachezwa kila siku, huku wenye bahati zao wakiendelea kujinyakulia vitita vyao vya Tatumzuka.Milard amewaasa Watanzania waendelee kucheza kwa wingi na mara kwa mara mchezo huo,kwani ukiibuka mshindi maisha yake huinuka na kuwa bora zaidi tofauti na alivyokuwa hapo awali.Mchezo wa kubahatisha wa TatuMzuka umetoa washindi wawili wa sh. Milioni 10 katika droo inayochezwa kila siku,mmoja akitokea jijini Dar na mwingine akitokea mkoani Kigoma
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka,Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka inayofanyika kila siku ,Harieth Steven (21) mkazi wa Kigoma ambaye anajishugulisha na kazi za ndani (housegirl),mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .
Harieth Mwenye mtoto mmoja alifurahia kujishindia donge hilo kupitia mchezo wa kubahatisha wa Tatumzuka,kwani baada ya kutaarifiwa kuwa amejishindia kiasi hicho cha fedha,akajipa matumaini ya kuwa ndoto yake ya kufanya biashara ya vitenge sasa inakwenda kutimia rasmi,na kuacha kufanya kazi za ndani.
Mmoja wa Maofisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Tatumzuka, Millard Ayo akimkabidhi mfano wa hundi ya sh.milioni 10 kwa mshindi wa droo ya Tatu Mzuka ,Ally Rashid (26) mkazi wa Yombo Buza ambaye anajishugulisha na biashara ya kuuza Mboga mboga jijini Dar,mapema leo kwenye mkutano na Wanahabari (hawapo pichani),uliofanyika leo jijini Dar .

No comments:

Post a Comment

Pages