HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 03, 2018

KANISA LA KKKT-BOKO WAWAKUMBUKA WATOTO WANAOUGUA SARATANI

Baadhi ya Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya kukabidhi zawadi za dawa, nguo na vifaa mbalimbali kwa watoto wanaougua saratani katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, wakiwa wamepozi kwa picha.
Baadhi ya wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, wakiwa wamepozi kwa picha.
Makamu Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sylvia Lupembe, akizungumza na wanawake wa usharika huo baada ya kuwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Makamu Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sylvia Lupembe, akizungumza na wanawake wa usharika huo baada ya kuwasili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Baadhi wa wanaumoja wakipeleka zawadi mbalimbali katika Wodi za Watoto.
Muuguzi aliyesajili, Baraka Mngóngó, akizungumza na Wanaumoja wa Wanawake wa KKKT Usharika wa Boko.
Wanaumoja wakipeleka zawadi katika Wodi za Watoto wanaougua saratani.
Ofisa Muuguzi wa Wodi za Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Asteria Henjewele, akiwashukuru wanaumoja hao  kwa zawadi mbalimbali zikiwemo dawa na nguo kwa watoto wanaougua saratani katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT-Boko.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Marry Lema, akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa watoto wanaougua kansa ambao wamelazwa katika Muhimbili.
Mwakilishi wa Wazazi akishukuru kwa niaba ya wazazi wenzake.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akifanya maombi.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akiwa amembeba watoto.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akiwa amembeba mmoja wa watoto waliolazwa katika hospitali hiyo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akiwaombea watoto wanaougua kansa.
Makamu Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Sylvia Lupembe, akizungumza katika makabidhiano hayo.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akimkabidhi Ofisa Muuguzi wa Wodi za Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Asteria Henjewele, zawadi za dawa, nguo na vifaa mbalimbali kwa watoto wanaougua saratani katika hospitali hiyo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake wa Kanisa hilo, Marry Lema.
Ofisa Muuguzi wa Wodi za Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Asteria Henjewele, akimshukuru Mwenyekiti wa Wanaumoja wa Wanawake wa Kanisa la KKKT Usharika wa Boko, Marry Lema.
Ofisa Muuguzi wa Wodi za Watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Asteria Henjewele, akitoa shukrani zake niaba ya uopngozi wa hospitali.
Mama Mchungaji, Janeth Nkini, akitoa zawadi kwa watoto waliolazwa katika wodi ya Upendo.
Picha ya pamoja.
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Boko, Hereld Nkini, akizungumza na Wanaumoja wa wanawake wa usharika huo baada ya kutoa zawadi kwa Watoto.
Wanaumoja wakiwa na furaha baada ya kumaliza kazi ya kutoa zawadi kwa watoto.
Baadhi ya wanaumoja wa Wanawake KKKT-Boko wakiwa wamepozi kwa picha.
Baadhi ya wanaumoja wa Wanawake KKKT-Boko wakiwa wamepozi kwa picha.
Picha ya pamoja. 

Na Mwandishi Wetu
 
KIKUNDI cha Wanawake kutoka Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Usharika wa Boko jijini Dar es Salaam, umekabidhi zawadi za dawa, nguo na vifaa mbalimbali kwa watoto wanaougua saratani.

Zawadi hizo zenye thamani ya Shs. Mill. 3 zilitolewa kwa watoto wanaotibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Kabla ya kukabidhi zawadi hizo, Mchungaji Kiongozi wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Usharika wa Boko, Hereld Nkini aliongoza maombi ya Baraka na uponyaji kwa wagonjwa hao.

Akizungumza kabla ya maombi hayo Mchungaji Nkini alisema zawadi hizo ni dalili za upendo kwa wagonjwa zenye lengo la kuwafariji huku akiwataka kumwamini Mungu katika mapito yao.

“Sisi sote ni wanadamu ila aliyetuumba ndiye anayetupitisha hapa tulipo leo, msikate tamaa, tumwamini na kumtumainia Mungu… japo tulichokileta leo ni kidogo kwa macho msikitizame hiki, tizameni upendo wetu kwenu.

“Kwenye Kitabu cha Mathayo 11:28 Biblia Takatifu inasema ‘Njoeni kwangu nyote msumbukao na kuelemewa na mizigo nami nitawapumzisha.’ Tukimbilie kwa Mungu ameahidi kutupa pumziko, magonjwa ni mizigo tuipeleke kwake akatupe pumziko,” alisisitiza Mchungaji Nkini.

Ofisa Muuguzi wa wodi hiyo Asteria Henjewele alisema zipo wodi tatu zenye wagonjwa tofauti huku akibainisha kwamba watoto wengi wanaotibiwa hapo wanasumbuliwa na saratani ya damu.

Henjewele alizitaja wodi hizo kuwa ni Upendo yenye wagonjwa wanaohitaji uangalizi wa karibu, Tumaini inayolaza wagonjwa wanaopata nafuu na Ujasiri ambayo ni hosteli inayotumiwa zaidi na wagonjwa wanaotoka nje ya Dar es Salaam ambao hawana uwezo wa kurudi kwao lakini wanaendelea na matibabu.

“Saratani ya damu imekuwa tatizo hasa kwa siku za karibuni… hapa kwetu hao ni wengi wakifuatiwa na wenye saratani ya macho na figo pia wachache wanaletwa kwa saratani ya matezi.

“Kwa mwezi tunapokea takribani wagonjwa 300 kati yao wapo wnaolazwa na wengine wanahudumiwa na kuondoka na changamoto zilizopo hapa ni dawa kwa wakati, na mahitaji mengine hasa kwa wagonjwa wanaotoka mikoani,” alisema Henjewelle.

Mwenyekiti wa Kikundi hicho, Mary Lema alisema zawadi hizo ni upendo wa wanawake hao kwa jamii huku akisisitiza kwamba wametoa wakati huu wa Kwaresma ili kusindikiza sala na maombi yao kwa Mungu.

“Huu ni wakati wa Kwaresma ni utaratibu wetu kutoa sadaka ama zawadi hii kwa wagonjwa kila mwaka lakini pia ukumbuke tunaelekea siku ya Wanawake Duniani…,” alisema Lema ambaye ni muuguzi kitaaluma.

No comments:

Post a Comment

Pages