Dande Contact

TEMBELEA BLOG HII KWA MATUKIO YA KILA SIKU-MOBILE +255 713 623 958 / +255 784 623 958 EMAIL dande15us@gmail.com

Halotel


CRDB

CRDB
.

Pages

PUMA ENERGY YAFADHILI MPANGO WA USALAMA BARABARANI KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI


Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akikata utepe kuashiria uzinduzi wa miundombinu ya usalama barabarani katika shule za Msingi Mikumi na Mzimuni ikiwa ni mwendelezo wa mpango wa uboreshaji wa usalama barababarani kwa wanafunzi wa shule za msingi jijini Dar es Salaam ambao unaratibiwa na shirika la Amend kwa ufadhili wa Mfuko wakampuni ya Puma Energy na Mfuko wa FIA. Wanaoshuhudia ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na maofisa wa Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akikabidhi msaada wa jaketi la usalama barabarani kwa mwanafunzi Nuru ambae ni Muhanga wa ajali za barabarani. Nuru alilazimika kukaa hospitali kwa kipindi cha miaka miwili akipatiwa matibabu baada ya kugongwa na gari maeneo jirani na shule hiyo.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akishirikiana na wanafunzi wenye ulemavu kutoka shule ya Gilman Rutihimaba kuimba nyimbo zenye mafunzo ya usalama barabarani.

Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti akizungumza kwenye hafla hiyo.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, walimu na wanafunzi wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na Wenye Ulemavu, Jenista Mhagama akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti, na maofisa wa shirika la Amend, Jeshi la Polisi kikosi cha usalama Barabarani, walimu wa shule za Msingi Mikumi na Mzimuni.

Waziri wa Kazi, Ajira, Sera, Bunge, Vijana na wenye ulemavu, Jenista Mhagama akigagua miundombinu ya usalama barabarani iliyojengwa kupitia mpango huo. Wengine ni pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania, Bw Philippe Corsaletti

No comments:

Post a Comment