HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2018

RAIS MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA RELI YA KISASA ITAKAYOTUMIA UMEME SGR-KUTOKA MOROGORO HADI MAKUTUPORA- DODOMA KM 422 KATIKA ENEO LA IHUMWA NJE KIDOGO YA MJI WA DODOMA

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa pamoja na Balozi wa Uingereza hapa nchini Sarah Cooke wakishuhudia.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa wakati akiweka jiwe la msingi ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa itakayotumia umeme Standard Gauge (SGR) itakayotoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma katika eneo la Stesheni ya Ihumwa nje kidogo ya mji wa Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akifunga kifuniko mara baada ya kutumbukiza karatasi ya majina ya viongozi mbalimbali waliofanikisha ujenzi huo kama kumbukumbu katika uwekaji wa jiwe la msingi la Reli ya Kisasa(SGR) itakayotoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa kutoka mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiweka saruji iliyochanganywa na kokoto kwenye jiwe hilo la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa mkoani Morogoro-hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
 Rais John Magufuli akikata utepe pamoja Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya umeme kutoka mkoani Morogoro hadi Makutupora Dodoma yenye urefu wa km 422 katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma jana. Wengine katika picha ni Naibu Spika Dk. Tulia Ackson, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa,  Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRC), Masanja Kadogosa pamoja na viongozi wengine.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua mfano wa Reli hiyo ya Kisasa itakayotumia umeme mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.
Treni ya zamani ikipita katika Reli za zamani katika eneo la Ihumwa stesheni mkoani Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa Shirika la Reli TRC Masanja Kadogosa akitoa maelezo ya mradi huo wa Reli ya kisasa ya umeme kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli. (PICHA NA IKULU).

No comments:

Post a Comment

Pages