HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

March 14, 2018

SEKRETARIETI YA TFF YAMPELEKA MICHAEL WAMBURA KAMATI YA MAADILI

Kamati ya maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF inakutana leo Jumatano Machi 14,2018 pamoja na mambo mengine kamati hiyo itajadili suala la Makamu wa Rais wa TFF Michael Richard Wambura aliyefikishwa kwenye kamati hiyo kwa masuala ya kimaadili.
Shauri hilo la Wambura limefikishwa kwenye kamati ya Maadili na Sekretarieti ya TFF baada ya Kamati ya Ukaguzi kukutana na kupitia mambo mbalimbali ya ukaguzi na suala hilo la Wambura kuonekana linatakiwa kufika kwenye Kamati ya Maadili.
Kamati ya Maadili imepokea malalamiko yanayomuhusu Wambura ikiwa ni uvunjifu wa kanuni za Maadili Tolea la 2013 na Katiba ya TFF kama ilivyorekebishwa mwaka 2015.
Wito huo umemtaka Wambura kufika mbele ya Kamati ya Maadili baadaye leo na ana hiyari ya kufika kutoa utetezi huo kwa njia ya mdomo,kutuma kwa maandishi,kuleta mashahidi au kutuma muwakilishi akiambatana na barua ya uwakilishi.
Makosa anayoshtakiwa Wambura ni
1.Kupokea/Kuchukuwa fedha za Shirikisho (TFF) za malipo ambayo hayakuwa halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(1) cha kanui za Maadili za TFF Toleo la 2013
2.Kughushi barua ya kueleza alipwe malipo ya Kampuni ya JEKC SYSTEM LIMITED huku akijua malipo hayo sio halali ikiwa ni kinyume na kifungu cha 73(7) cha Kanuni za Maadili za TFF Toleo la 2013
3.Kufanya Vitendo vinavyoshusha hadhi ya Shirikisho ikiwa ni kinyume na Ibara ya 50(1) ya Katiba ya TFF (Kama ilivyorekebishwa 2015)

AMMY NINJE KOCHA NGORONGORO HEROES
Kocha Ammy Ninje ameteuliwa kuwa Kocha wa muda wa Timu ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya miaka 20(Ngorongoro Heroes)
Ninje atakiongoza kikosi hicho kwakuwa Kim Poulsen na Oscar Mirambo wamebaki na majukumu na kikosi cha Timu ya Taifa chini ya miaka 16 Serengeti Boys kinachojiandaa na mashindano ya Cecafa yatakayoanza Aprili 1-15,2018 nchini Burundi.
Kocha Ninje atakiongoza kikosi cha Ngorongoro Heroes kuanzia kwenye mechi zake za Kirafiki za Kimataifa dhidi ya Morocco Machi 17,2018,dhidi ya Msumbuji Machi 21,2018 na mchezo wa kufuzu fainali za Africa kwa Vijana chini ya miaka 20 dhidi ya DR Congo zote zikichezwa Uwanja wa Taifa.
Mshindi kati ya Tanzania na DR Congo atakwenda kucheza na Mali katika raundi ya pili itakayochezwa mwezi Mei.
Awali Ninje alikuwa kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya wakubwa Taifa Stars ambapo pia alikuwa kocha mkuu wa Kilimanjaro Stars kwenye mashindano ya Kombe la Chalenji yaliyofanyika nchini Kenya.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA TFF.

No comments:

Post a Comment

Pages