Rais
huyo wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) jana Machi 14, 2018
alifanyiwa upasuaji wa mguu wa kulia kama alivyoshauriwa na madaktari wa
Hospitali ya Chuo Kikuu cha Leuven, Gasthuisberg nchini Ubelgiji.
Akizungumza
leo na Mwananchi Machi 15, 2018, Lissu amesema operesheni hiyo
iliyochukua saa mbili ilifanywa na timu ya madaktari bingwa chini ya
uongozi wa Profesa Willem-Jan Mertsemakers.
“Operesheni
ilienda vizuri na kwa sasa naendelea na dawa na mapumziko hospitalini
kwa muda wa angalau wiki tatu zinazokuja,” amesema Lissu.
“Wameniwekea
chuma cha kuimarisha mfupa wote wa paja la kulia. Pia wamechukua vipimo
ili kuangalia kama hakuna tatizo la bacteria kabla hawajafunga kabisa
sehemu ya kwenye goti ambayo haijaunga hadi sasa.”
Mke wa Lissu, Alicia amesema anamshukuru Mungu kwamba upasuaji huo umekwenda vyema. Chanzo Mwananchi.
No comments:
Post a Comment