Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji
Charles Mwijage mara baada ya kufungua kiwanda cha Sigara cha Mansoor
Industries ltd kilichopo chini ya leseni ya Phillip Morris Tanzania katika eneo
la Kingolwira mkoani Morogoro. Wa kwanza kushoto ni Meneja Mkuu wa Kiwanda cha
Phillip Morris Tanzania Dagmara Piasecka akipiga makofi, wengine katika picha
ni Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe pamoja na Mmiliki wa kiwanda cha
Sigara Mansoor Shanif Hirani.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikagua
Tumbaku inayotumika katika utengenezaji wa Sigara hizo za Marlboro mara baada
kufungua kiwanda hicho cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
mapakiti ya sigara hizo za Marlboro wakati akikagua utendaji kazi wa shughuli
mbalimbali za kiwanda hicho mara baada ya kukifungua.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
mojawapo ya hatua katika utengenezaji wa Sigara mara baada ya kufungua kiwanda
hicho mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia
mojawapo ya vifungashio vya Sigara hizo kiwandani hapo mara baada ya
kukifungua.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia
mkono wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha
Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Msanii mkongwe Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya
kuhutubia wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara
cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na wananchi waliofika katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha
Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na Chifu Kingalu Mwanabanzi wa Kabila la Waluguru wa Morogoro mara
baada ya kumaliza kuzungumza na wananchi waliofika katika kiwanda cha Sigara
cha Mansoor kilichopo Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Steven Kebwe mara baada ya kuzindua
kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
Msanii
mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle akitumbuiza katika
sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara mkoani Morogoro.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimsalimia
mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa Mama
Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya
biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro.
Mfanyabiashara mdogo (Machinga) wa Mama
Havintoshi ambaye aliwasilisha kero yake ya kunyanyaswa wakati akifanya
biashara zake katika stendi ya daladala ya mjini Morogoro akichangiwa fedha na
wadau mbalimbali mara baada ya kero yake kupatiwa ufumbuzi na Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais John Magufuli akimpongeza
Msanii mkongwe wa Bongo flavour Selemani Msindi au Afande Selle mara baada ya
kutoa burudani ya mziki na kutangaza rasmi kuhamia katika Chama cha Mapinduzi
CCM katika sherehe za ufunguzi wa kiwanda cha Sigara cha Mansoor kilichopo
Kingolwira mkoani Morogoro.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
jambo na Mmiliki wa kiwanda hicho cha Sigara Mansoor Shanif Hirani mara baada
kufungua kiwanda hicho. PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment