WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemkabidhi Bibi Tecla Hamidu ambaye ni mlemavu wa miguu sh. milioni tano ili
aweze kuongezea katika mtaji wake.
Ametoa fedha hizo leo (Jumanne, Machi
20, 2018) ikiwa ni katika kutimiza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2018
kwenye Mkutano wa Sita wa Wamiliki wa Viwanda na Watumiaji wa
simbomilia (barcodes).
Waziri Mkuu alitoa ahadi hiyo baada ya Bibi
Tecla ambaye ni mjasiriamali anayejihusisha na ushonaji wa bidhaa mbalimbali
zikiwemo nguo kumuomba amchangie sh. 500,000 ili aweze kuongezea mtaji wake.
Wakati akimkabidhi fedha hizo, Waziri
Mkuu amesema kwamba anatarajia zitamsaidia katika kuongeza mtaji wake, hivyo atazalisha bidhaa nyingi
zenye ubora unaohitajika katika masoko ya ndani na nje.
Kwa upande wake, Bibi Tecla
alimshukuru Waziri Mkuu kwa msaada huo na ameahidi kuzitumia fedha hizo kama
ilivyo kusudiwa.
“Nashukuru kwa msaada huu kwani kuna
watu wanakopa sh. laki mbili ili waongeze mitaji, lakini mimi leo nimepewa
milioni tano bure na kiongozi wetu,”
Amesema licha ya kukabiliwa na
changamoto ya upatikanaji wa masoko anaamini tatizo hilo litakuwa historia
baada ya kuwa na mtaji wa kutosha kwani atakwenda kuzalisha bidhaa zenye ubora
zaidi.
IMETOLEWA NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE,
MACHI 20, 2018.
No comments:
Post a Comment