HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 20, 2018

MSIFANYE KAZI KWA MASHINDANO NA WANASIASA; JAJI MKUU ZANZIBARA

JAJI MKUU wa Zanzibar, Omar Othman Makungu, Katika amewataka, mahakimu  wasifanye kazi  kwa mashindikizo ya wanasiasa, kwani  wakifanya hivyo watakuwa hawaitendei haki fani yao.

Jaji huyo alieleza hayo kwa nyakati tofauti, alipokuwa akizungumza na watendaji wa mahakama za mwanzo Wingwi, Konde na Wete, ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku nne kisiwani  Pemba.

 Alieleza kuwa umefika muda Mahakimu wafanye kazi zao kisayansi na kuacha mashindikizo ambayo yataharibu uwaminifu wao kwa jamii.


“Lazima muelewa mahakimu wetu kwamba, kuna kupanda daraja kwa mujibu wa kazi zenu, lakini kama mnafanyakazia kwa chuki, mashindikizo basi msitarajie kupanda ngazi,”alieleza Jaji Makungu.

Sambamba na hilo aliwauliza mahakimu kisiwani humo, wamezitoa wapi sheria zinazowapa mamlaka ya kuwalazimisha watuhumiwa kuwa na wafanyakazi wa serikali au barua za masheha wanapoomba dhamana dhidi ya kesi zinazowakabili.

Alisema anashangaa kuona baadhi ya mahakimu hao, kuwawekea masharti magumu watuhumiwa, kwa lengo la kutafuta sababu ya kuwapelekea rumande, jambo ambalo sio sahihi maana huko sio kwahali kwema kwa kukaa
mwanadamu.


Alisema lazima mahakimu wafahamu  kuwa, kumpeleka mtuhumiwa rumande ni hatua ya mwisho, na sio iwe ndio kipaumbele chao, kwa kuwekea masharti magumu au kima kikubwa cha fedha.

Alieleza kuwa, yeye binafsi hajaona popote kwenye sheria, kuwa mtuhumiwa anatakiwa ili kutimiza masharti kwambaawe na mtu anaefanyakazi serikalini, au barua ya sheha kwamba ndio kigezo namtuhumiwa akishindwa na hayo, apelekwe rumade.

“Jamani wale ni binadamu, wapo waliotenda makosa, wapo walioteleza nawengine wamesingiziwa  sasa na nyinyi mkishawishika kwa kuwapeleka rumade,  tena kwa mashartimazgumu,mtakuwa mtakuwa hamukuwatendea haki” alieleza jaji Makung

Nae Mrajisi wa jimbo mahakama kuu Pemba Hussein Makame Hussein, alisema changamoto kadhaa wamezisikia hawa walipowatembelea wanafunzi,
juu ya kucheleweshea mienendo ya kesi, jambo kwa sasa wanajitahidi kuliepuka.

Ziara ya Jaji Mkuu Zanzibar akiwa na Mrajisi na Manaibu Warajisi, itaendelea tena kesho kwa kulikagua jengo la Mahakama Kuu Chakechakeya kuzungumza na watendaji wake, na kukamilisha ziara yake ya Siku Nne kisiwani humo.

No comments:

Post a Comment

Pages