HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 29, 2018

Benki ya CRDB yapunguza riba, marejesho miaka saba

 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akitangaza kupunguza riba za mikopo ya benki hiyo kutoka asilimia 22 hadi 16 na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka saba. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Meneja wa SME wa CRDB, Elibariki Masuke.
 Dk. Kimei akizungumza na waandishi wa habari.
 Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kazini.

NA MWANDISHI WETU

BENKI ya CRDB imepunguza kiwango cha riba ya mikopo yake kutoka asilimia 22 hadi asilimia 16 na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka saba kwa wafanyakazi.

Pamoja na hayo benki hiyo inayomsikiliza mteja, imeongeza ukomo wa mkopo kutoka Sh. milioni 50 za awali hadi Sh. milioni 100 ambazo mkopaji anaweza kuzipata ndani ya saa 12 za kazi baada ya kukamilisha nyaraka za maombi ya mkopo wake.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei alisema lengo la benki hiyo ni kuwanufaisha wafanyakazi na kuwahamasisha waanzishe miradi mingine ya maendeleo ili kukuza uchumi wa nchi.

"Tumesikia wito na ushauri wa Rais wetu John Magufuli wa kupunguza kiasi cha riba kwenye mikopo yetu nasi tumefanya hivyo lakini pia tunamhamasisha mfanyakazi kwamba asiendelee kutegemea ajira tu afanye na biashara nyingine ili ajiandae kustaafu, anakuja kwetu tunampa Sh. milioni 100 ananunua magari anayafanya Uba anapata kipato cha ziada.

"Nawashauri msije kukopa mkaenda kufanya harusi... kopeni kwa maelengo ili wakati wa marejesho mshahara ukikatwa lakini kuna hela nyingine inaingia," alisema Dk. Kimei na kutangaza kununua mikopo ya wafanyakazi waliyokopa kwenye taasisi nyingine.

No comments:

Post a Comment

Pages