Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wageni
mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi walioshiriki katika futari aliyowaandalia
Ikulu jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa akiwa amekaa na Rais
mstaafu wa awamu ya Tatu Benjamin Mkapa wa pili kutoka kulia, Rais mstaafu wa
awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mstaafu Dkt. Mohamed Gharib
Bilal pamoja na viongozi mbalimbali walioshiriki Futari iliyoandaliwa na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es
Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein pamoja na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakary Zubery mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar es Salaam. wa pili kutoka kulia ni Waziri wa Dini kutoka Saudia Arabia Dkt. Saleh Abdulaziz Alashek
Wageni
mbalimbali wakiwemo viongozi wastaafu pia walishiriki katika futari hiyo.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais
mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi mara baada ya kufuru Ikulu jijini
Dar es Salaam.
Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais
mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa mara baada ya kufuturu Ikulu jijini Dar
es Salam. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment