Watangazaji Nguli
Kurindima kwa Kiswahili
Wateja kutazama popote
walipo
Mtanange huo kuonyeshwa
live kwenye vifurushi vyote
Channel maalum 6
kuonyesha Michuano hiyo katika HD
Dar es Salaam, Tanzania
Huku zikiwa zimebaki siku chache kwa kinyang’anyiro cha Kombe la
Dunia 2018 kuanza nchini Urusi, Kampuni
ya MultiChoice Tanzania imetangaza neema kwa Watanzania kwa kutoa ofa maalum
kwa wateja wapya, huku ikitenga chaneli 6 maalum zitakazoonyesha michuano hiyo
katika kiwango cha HD pamoja na kuwawezesha wateja wake wote kufuatilia
michuano hiyo kwa Lugha ya Kiswahili katika vifurushi vyote vya DStv.
“Hii ni zaidi ya ofa” anasema Ronald
Shelukindo, Mkuu wa Uendeshaji wa MultiChoice Tanzania wakati akitangaza ofa
hiyo jijini Dar es Salaam jana. “Sasa tunataka watanzania waweze kupata
burudani ya kombe la dunia 2018 kwa namna tofauti kabisa. Kwanza kwa wateja
wapya wataweza kujiunga kw shilingi 79,000 tu na kupata seti ya DStv pamoja na
kifurushi cha miezi miwili bure!” alisema Shelukindo na kuongeza “Kama hiyo
haitoshi, wateja wote wa DStv, sasa wataweza kupokea matangazo ya moja kwa moja
kwa lugha ya Kiswahili ambapo tuna timu ya watangazaji mahiri wa soka hapa
nchini watakaowaletea watanzania burudani hii”
Amesema mbali na ofa hiyo na kutangazwa kwa
michuano hiyo kwa lugha ya Kiswahili, pia DStv imetenga chaneli 6 mahususi
kabisa kwa ajili ya michuano hiyo pamoja na kuhakikisha kuwa wateja wanaweza
kutazama DStv popote walipo wakati wowote kwa kutumia vifaa kama simu, laptop
na tablet. “Hivi sasa ukipakua app yetu ya DStv Now, unaweza kutumia hadi vifaa
vitano tofauti ambavyo vyote huunganishwa na dikoda yako hivyo kuwawezesha
wanafamilia kutazama vipindi tofauti kwa wakati mmoja” alisema Shelukindo.
Akitoa maelezo kuhusu jinsi DStv
ilivyojizatiti kuwahakikishia watanzania burudani isiyo na kifani msimu huu wa
kombe la dunia, Mkuu wa Masoko wa MultiChoice Tanzania Alpha Mria, amebainisha
kuwa DStv itaonyesha michuano hiyo katika vifurushi vyake vyote, hivyo wateja
wote wa DStv watafurahia michuano hiyo tena katika muonekano angavu yanni HD.
“Kwakeli msimu huu wa kombe la Dunia, kila
atakayekuwa na DStv atakuwa anapata hasa kile anachostahili kwani mechi zote
zitaonekana live, kwenye HD na kwenye vifurushi vyote, huku pia zikitangazwa
kwa lugha mbalimbali ikiwemo lugha ya Kiswahili” alisema Alpha
Amesema kwa wale wanaotaka kufuatilia kwa
Kiingereza wataweza kuona kupitia DStv, wale wa Kireno wataona kupitia DStv,
wale wa Kifaransa pia wataona kupitia DStv, na kikubwa zaid sisi watanzania
tutaweza kufuatilia kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili kupitia DStv.
“Tumejipanga, kuwapa watanzania burudani ya aina yake msimu huu wa kombe la
Dunia” Alisisitiza Alpha.
Katika uzinduzi huo, DStv iliwatambulisha
rasmi watangazaji wa soka ambao watakuwa wakiwaletea watanzania matangazo hayo
kwa Kiswahili ambapo majina makubwa ya watangazaji na wachambuzi wa soka yamo.
Waliotambulishwa ni Aboubakary Liongo, Maulid Kitenge, Ephaim Kibonde, Edo
Kumwembe, Ibrahim Masoud - Maestro na Oscar Oscar.
Wakiongea baada ya kutambulishwa, watangazaji
na wachambuzi hao mahiri wa soka wamesema wamejizatiti kikamilifu kuhakikisha
kuwa wanawaletea matangazo na uchambuzi wa kina ili kuhakikisha kuwa kila
mpenda soka anafurahia na kuyaelewa vizuri mashindano hayo.
“Mwaka huu mtoto hatumwi sokoni. Kwa DStv,
hii ni zaidi ya kombe la Dunia kwani tutakuwa tukiwaletea uchambuzi wa kina
kabla, wakati na baada ya mechi. Bila shaka itakuwa ni burudani mwanzo mwisho”
alikaririwa Maulid Kitenge, mmoja kati ya watangazaji hao.
Uzinduzi
huo ulihudhuria na mamia ya wadau mbalimbali wa soka nchini wakiwemo wachezaji
maarufu waliochezea timu mbalimbali pamoja na timu ya Taifa pamoja ni viongozi
mbalimbali na wapenzi wa soka maarufu nchini. Pia wachezaji kadhaa wa klabu za
Simba na Yanga walihudhuria hafla hiyo iliyokuwa ya kufana sana
No comments:
Post a Comment