HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 23, 2018

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI AWATEMBELEA WANANCHI JAMII YA WAHADZABE

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh  kijiji cha Dumanga Yaeda Chini wilayani Mbulu mkoa wa Manyara wakati alipozitembelea jamii hizo ili kuzungumza nao kuhusu maisha yao pamoja na uhifazi wa tamaduni na mila zao ambao unaweza kuwa Kivutio cha Utalii pia lakini pia kujua mahitaji yao ya muhimu katika maisha ya jamii hizo.(PICHA NA JOHN BUKUKU FULLSHANGWE-MBULU)
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na wananchi wa jamii za Wahdzabe Watatoga na Wasukuma wakati alipotembelea Kata ya Eshkesh  kijiji cha Dumanga kutoka kulia ni Gesso Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu., Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduzi Wizara ya habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Beleko na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.
 Wananchi wa Eshkesh Jamii ya Watatoga wakiwa katika mkutano huo.
 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga akizungumza katika mkutano huo.
 Gesso Bajuta diwani wa kata ya Endamilay wilayani Mbulu akizungumza katika mkutano huo.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimtunza mmoja wa vijana aliyekuwa akicheza ngoma ya kisukuma katika mkutano huo.
 Mmoja wa vijana  wapiga ngoma akipiga ngoma kwa mbwembwe wakati kikundi cha ngoma ya kisukuma kikitumbuiza.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu Bw. Hudson Kamoga.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan katikati  na Kaimu Mkurugenzi wa Utamaduni Wizara ya Habari Sanaa na Utamaduni Bi. Liliano Beleko wa pili kutoka kushoto wakicheza ngoma na akina mama wa jamiii ya Wahadzabe katika kijiji cha Dumanga.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akimpa pole mama aliyejifungua na kupoteza mwanaye alifariki baada ya kuzaliw.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akizungumza na Mmoja wa akina mama wa kihazabe nyumbani kwake Jamii ya Wahadzabe wananawake ndiyo wanaojenga nyumba kazi ya wanaume ni kuwinda wanyama na  kurina asali pamoja na kutafuta mizizi kwa ajili ya chakula.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akitoka katika moja ya nyumba ya familia ya kihdzabe.
  Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akifurahia jambo baada ya kuvaliswa zawadi ya mkanda uliotengenezwa kwa Shanga na Bi.Chrstina Paulo mama wa jamii ya Kihadzabe.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi akivishwa mkanda uliotengenezwa kwa Shanga na Bi.Chrstina Paulo mama wa jamii ya Kihadzabe.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakikimbia na akina mama wa Kihadzabe huku wakiimba kuelekea eneo la makazi yao mara baada ya kupokelewa.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakicheza na akina mama wa Kihadzabe huku wakiimba kuelekea eneo la makazi yao mara baada ya kupokelewa.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakipokelewa na wananchi wa Dumanga wa jamii ya Kitatoga mara baada ya kuwasili kijijini hapo.
   Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi. Suzan Mlawi na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Mbulu wakipokelewa na ngoma ya akina mama wa Kihadzabe.
 Vijana wa Kitatoga wakiimba katika mapokezi hayo.

No comments:

Post a Comment

Pages