Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa
Tanga, Lilian Mwalongo (kulia), akimkabidhi Jeremiah Mwamlenga
zawadi ya simu anja yenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 baada ya kuibuka
kama moja wa washindi wa promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus inayoendeshwa
na kampuni ya Tigo. Jumla ya washindi 996 wamepatikana katika promosheni
hiyo.
Meneja
Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia), akimkabidhi,
Mwanaisha Bakari zawadi ya simu Janja yenye uwezo wa 4G aina
ya Tecno R6. Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo (kulia) akimkabidhi Nuhu Munhambo zawadi ya simu Janja.
Tanga, Mei 15, 2018, Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali ya Tigo Tanzania, imewazawadia washindi 996 kutoka sehemu mbali mbali nchini simu za zenye uwezo wa 4G aina ya Tecno R6 katika promosheni yake inayoendelea ya Nyaka Nyaka Bonus
Akikabidhi zawadi kwa washindi 11 jiijini Tanga leo, Meneja Masoko wa Tigo, Mkoa wa Tanga Lilian Mwalongo alibainisha kuwa kupitia promosheni ya Nyaka Nyaka Bonus, Tigo itaongeza idadi ya watumiaji wa simu za kisasa pamoja na matumizi ya data nchini.
‘Ofa hii kabambe ni sehemu ya ubunifu wa Tigo unaoendana na mahitaji ya wateja na utakaowezesha kila mtu kufurahia huduma bora za mtandao wa Tigo 4G wenye kasi zaidi na ulioenea zaidi nchini,’ alisema.
Katika promosheni hiyo murwa ya Nyaka Nyaka Bonus, wateja wote wa Tigo wanaonunua bando za data kuanzia TZS 1,000 kupitia menu iliyoboreshwa ya *147*00# wanapokea bonasi ya hadi 1GB intaneti bure papo kwa hapo kwa matumizi ya Facebook, WhatsApp, Instagram ama Twitter. Pamoja na hayo, wateja pia wanapata nafasi ya kushinda mojawapo ya simu janja zenye uwezo wa 4G aina ya TECNO R6 ambazo zinatolewa bure na Tigo
No comments:
Post a Comment