HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 31, 2018

MultiChoice Yawekeza kukuza tasnia ya filamu Afrika

Programuya MultiChoice Talent Factory kuchochea ubunifu
· Watanzania kwenda mafunzoni mwaka mzima
· Wanaotaka kushiriki sasa milango iko wazi! 


DODOMA 30 Mei 2018 MultiChoice Africa, Imezindua rasmi program kubwa ya kijamii inayolenga kuleta mapinduzi makubwa katika tasnia ya filamu hapa Tanzania na barani Afrika kwa ujumla.

Program hiyo ijulikanayo kama MultiChoice Talent Factory (MTF) – inalenga kuchochea ubunifu wa vijana wa Afrika katika tasnia ya filamu na imeandaa vyuo maalum vitatu ambavyo vitatoa mafunzo maalum ya utengenezaji wa filamu kwa vijana kutoka nchi mbalimbali kote barani Afrika.

“Maendeleo ya nchi yetu kwa muda mrefu yamekuwa yakitambuliwa kwa uwekezaji katika maliasili nyingi tulizonazo kama vile madini, kilimo, mifugo, wanyamapori, na kadhalika huku sekta ya ubunifu ikiwa haijapewa kipaumbele kikubwa na hivyo sekta ya sanaa na ubunifu kuwa na mchango mdogo katika ukuaji wa uchumi wetu.
Ili kuhakikisha kuwa tunasaidiana na serikali katika mkakati wake wa kuifanya sekta ya ubunifu na sanaa kuwa moja ya mihimili ya uchumi wetu, MultiChoice imeanzisha program hii na tumeanza na sekta ya filamu” alisema Maharage Chande, Mkurugenzi wa MultiChoice kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi.

Tumebarikiwa kwa vipaji vingi katika fani mbalimbali na bila shaka tukiwekeza katika vipaji vya vijana wetu bila shaka tutafanikiwa kupanua wigo wa ajira na uchumi wetu na hivyo kuchangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.

Amesema Programmu hiyo itakayoanza rasmi mwezi Oktoba mwaka huu itawawezesha vijana wanne kutoka Tanzania kuungana na vijana wengine kutoka nchi mbali mbali za Afrika katika vyuo maalum vya mafunzo ya utengenezaji wa filam ambavyo vitakuwa nchini Nigeria, Kenya na Zambia.

Kwa upande wake, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe amesema program hiyo itakuwa chachu kubwa katika kuleta mapinduzi kwenye tasnia ya filamu hapa nchini kwani vijana watakaopatikana mbali na kwamba watakuwa na uwezo wa hali ya juu wa kutengeneza filamu, pali pia watakuwa kama waalimu wa wezao ambao wanavipaji katika tasnia hiyo.

“Nimefurahi sana kusikia kuwa MultiChoice wanapanga kuendelea na mpango huu kwa muda mrefu kwahiyo japokuwa tunaaza kwa kupeleka wanafunzi wanne, bado tunaamini huu ni mwanzo mzuri sana. Cha msingi kwanza siyo ididi ya wanafunzi, bali ni umuhimu wa chuo hicho na kiwango cha mafuzo kitakachotolewa. Tunaamini kwa mwaka huu wa kwanza vijana hao wakikamilisha mafuzo yao na wakirudi nyumbani watakuwa chachu kubwa katika kukuza na kuimarisha tasnia ya filamu hapa nchini”

Pia ametoa rai kwa MultiChoice kushirikiana kwa karibu na wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi na pia vyou vyetu ambavyo vinatoa elimu ya sanaa ya filamu ili kuhakikisha kuwa wanabadilishana ujuzi na uzoefu na pia ikiwezekana kuwa na miradi ya pamoja ya muda mrefu na mfupi na hivyo kuwafikia vijana wengi zaidi na kuweza kutimiza lengo kuu la kuifanya fani ya filamu kuwa moja ya nguzo za uchumi wa nchi hii.

Program hiyo inaanza rasmi kwa kupokea maombi ya washiriki ambayo yatapokewa kwa njia ya mtandao.
Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi Maharage Chande akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa programu ya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoa fursa kwa vijana wenye kipaji katika tasnia ya filamu kujiunga na kituo maalum cha mafunzo ya fani hiyo kwa muda wa mwaka mzima kwa udhamini wa MultiChoice Afrika. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi Maharage Chande akimkaribisha Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Tulia Ackson katika hafla ya uzinduzi rasmi wa programu ya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoa fursa kwa vijana wenye kipaji katika tasnia ya filamu kujiunga na kituo maalum cha mafunzo ya fani hiyo kwa muda wa mwaka mzima kwa udhamini wa MultiChoice Afrika. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma leo Mei 31, 2018.
Naibu Spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson (katikati), Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe (kulia) na Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi, Maharage Chande wakishuhudia uzinduzi rasmi wa programu ya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoa fursa kwa vijana wenye kipaji katika tasnia ya filamu kujiunga na kituo maalum cha mafunzo ya fani hiyo kwa muda wa mwaka mzima kwa udhamini wa MultiChoice Afrika. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma.
Naibu spika wa Bunge Dk. Tulia Ackson (wa nne kulia) Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dr. Harison Mwakyembe (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa MultiChoice Africa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi Maharage Chande (wa nne kushoto) pamoja na Naibu waziri – Kazi vijana na jira Anthony Mavunde (wa pili kulia), Naibu Waziri–Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa kamati ya Bunge – Maendeleo ya Jamii Peter Serukamba, (wa tatu kushoto), Katibu Mkuu – Habari Utamaduni Sanaa na Michezeo Suzan Mlawi (kulia) na Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania Joyce Fisoo (kushoto)  wakifurahi pamoja baada ya uzinduzi rasmi wa programu ya ‘MultiChoice Talent Factory’ inayotoa fursa kwa vijana wenye kipaji katika tasnia ya filamu kujiunga na kituo maalum cha mafunzo ya fani hiyo kwa muda wa mwaka mzima kwa udhamini wa MultiChoice Afrika. Uzinduzi huo ulifanyika jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Pages