Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Mufti Mkuu wa
Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir wakati alipowasili kwenye ukumbi wa
Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es
salaam kuwa mgeni rasmi katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Quraan
Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania, Mei
26, 2018. (Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kombo Faki Hamadi kutoka Pemba zawadi ya Shilingi milioni 4 baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa Juzuu 30 katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania ( Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam waliohudhuria katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakary Zubeir akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi Kombo Faki Hamadi kutoka Pemba zawadi ya Shilingi milioni 4 baada ya kuibuka kuwa mshindi wa kwanza wa Juzuu 30 katika Mashindano ya Kitaifa ya Kuhifadhi Qur-aan Tukufu yaliyofanyika kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Mei 26, 2018. Katikati ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania (Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kiislam ya Istiquaama Tanzania ( Istiqaama Muslim Community of Tanzania), Seif Ali Seif.
Baadhi ya washiriki wa Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagana na baadhi ya viongozi wa Taasisi na Jumuiya za Kiislam waliohudhuria katika Mashindano ya Kitaifa ya kuhifadhi Qur-aan Tukufu.
Dar es Salaam, Tanzania-WAZIRI MKUU Kassim
Majaliwa amewataka waumini wa dini ya Kiislamu wajiepushe na vitendo vinavyoweza
kupandikiza chuki dhidi yao au kwa waumini wa dini nyingine.
Ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi,
Mei 26, 2018) wakati akizungumza na viongozi na mamia ya waumini wa dini ya
Kiislamu walioshiriki mashindano ya kitaifa ya kuhifadhi Quran tukufu kwenye ukumbi
wa Mwl. J. K. Nyerere jijini Dar es Salaam.
Mashindano hayo
yaliyoandaliwa na Jumuiya ya Kiislamu ya Istiqaama Tanzania (Istiqaama Muslim
Community of Tanzania), yalijumuisha washiriki 29 kutoka mikoa mbalimbali ya
Tanzania Bara na Visiwani.
“Serikali inatambua na
inathamini sana, mchango wa dini katika kuwalea waumini kiimani na kutunza
amani ya nchi. Hivyo, tujiepushe na kauli au vitendo ambavyo vinaweza
kupandikiza chuki na uhasama dhidi yetu au dhidi ya waumini wa imani nyingine,”
amesema.
“Nitoe rai kwenu viongozi
wangu na waumini wenzangu, tujenge misingi ya kuvumiliana na kustahamiliana.
Hilo pekee ndilo linaloisimamisha nchi yetu kuwa ni mfano wa kuigwa na kimbilio
la wale waliovurugikiwa na amani katika nchi zao. Kadhalika, amani inajenga na
kutoa fursa ya kuweza kutekeleza majukumu yetu ya kiibada, kiuchumi na kijamii
bila hofu,” amesema.
Waziri Mkuu amesema
kwa mujibu wa Surah Al-Imraan Ayah 103, Allah Mtukufu alihimiza umuhimu wa
umoja miongoni mwa Waislamu. “Katika umoja huo, Allah amesisitiza Waislamu kuwa
wamoja na kutofarakana. Mafundisho na wasia wa Mtume Muhammad Swalla Allahu
Alayh Wasallam ni kuwa tupendane na tushikamane. Wakati wote Mtume wetu
aliheshimu na kuwathamini watu wote hata ambao hawakuwa Waislamu,” ameongeza.
“Kwa msingi huo, kama Waislamu
nasi ni vema tukajipamba na tabia njema za Mtume wetu Muhammad Swalla Allahu
Alayh Wasallam. Katika hili, mtakubaliana nami kuwa tabia njema ni miongoni mwa
makusudio muhimu sana ya kuletwa Mtume Muhammad kwetu,” amesema.
Katika
hatua nyingine, Waziri Mkuu amesisitiza umuhimu wa kuwapa elimu watoto
kama ambavyo imesisitizwa kwenye Quran tukufu na kama ambavyo imesisitizwa na
mafundisho ya Mtume Muhammad (SAW) kwamba suala la kutafuta elimu ni la lazima kwa
muislamu, awe mwanaume au mwanamke.
“Kama mnavyofahamu, Uislamu
umeweka mkazo mkubwa sambamba na kusisitiza umuhimu wa elimu. Hili
linathibitishwa na aya ya kwanza kabisa ya Quran kuteremshwa kwa Bwana Mtume
Muhammad Swalla Allahu Alayh Wasallam (SAW) ambayo ilimuamrisha kusoma (Surah
Al-’Alaq ayah 1).”
“Kwa msingi huo, kama
ambavyo mnatoa msukumo kwa vijana wetu kusomeshwa Quran, msukumo huo huo muutoe
pia katika kuhakikisha kuwa vijana hawa wanapatiwa mafunzo sahihi kuhusu tabia
njema, utii na kuheshimu mamlaka za utawala zilizopo. Kwa kufanya hivyo,
tutawasaidia vijana hawa kuwa raia wema na wazalendo kwa nchi yao,” amesema.
Amesema Quran licha ya
kuwa ni kitabu cha dini lakini kimebeba masuala yote muhimu katika maisha ya muislamu
ya kila siku. “Hivyo, ukitaka kuleta maendeleo ya uchumi ulio imara, ukitaka
kujenga jamii inayoheshimu na kufuata misingi ya uadilifu, ukitaka kujenga Taifa
lenye amani na utulivu, huna budi kuwekeza zaidi katika elimu. Kwa hiyo,
uwekezaji katika elimu haumaanishi tu kuhakikisha watoto wetu wanasoma na
kuhifadhi Quran pekee, bali pia wanapaswa kupewa fursa ya kujifunza elimu ya
mazingira ili waweze kufikia hatua bora za kimaisha duniani na akhera,” amesema.
Kwa
upande wake, Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubei alisema mashindano
hayo yamefana na imeshangaza kuona mtoto anatajiwa namba tu ya aya na anaweza
kuielezea kuwa iko kwenye sura fulani.
Kama ambavyo nabii
Yahya aliamriwa kushika kitabu, nasi pia tushike kitabu na tuyashike yaliyo ndani
yake, tusije kuishi katika ardhi yenye rutuba na yenye rasilmali madini halafu
na sisi tushindwe kuvuna kile kilichomo,” alisema.
Naye Mwenyekiti
wa Jumuiaya ya Istiqaama Tanzania, Sheikh Seif Ally Seif alisema jumuiya hiyo yenye
matawi 20 Tanzania Bara na Visiwani, ilianzishwa mwaka 1993 kwa lengo la kutoa
mafunzo ya kiroho na kuwajengea vijana maadili mema ili Taifa liwe na watu
wenye kujali amani, wanaoheshimiana na kupendana kidugu.
Alisema jumuiya hiyo
imejenga shule 14 za msingi na sekondari kwenye maeneo mbalimbali nchini na
inatarajia kujenga shule kubwa ya kimataifa jijini Dar es Salaam ikiwa ni
pamoja na kufungua shule ya ufundi.
Katika mashindano
hayo, kijana Kombo Fakhi Hamad (19) kutoka Istiqaama Pemba aliibuka mshindi wa
jumla kwa kuweza kuhifadhi juzuu 30 na kupewa zawadi ya sh. milioni nne. Kombo pia
aliibuka mshindi wa kwanza kwenye kundi la kuhifadhi juzuu 30 (tahfidh)
akifuatiwa na Ally Said Mohamad (18) aliyepata sh. milioni mbili. Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na Mariam Nassor Said (14) aliyepata sh. milioni 1.5.
Katika kundi la kuhifadhi
juzuu 30 (tashdia), Masoud Bakari Ally (18) alikuwa mshindi wa kwanza na
alipewa zawadi ya sh. milioni moja akifuatiwa na Mustafa Abdallah Hamad (17) aliyepata
sh. 700,000 na wa tatu alikuwa Jumaa Ally Othman (16) aliyepata sh. 500,000.
Katika
kundi la kuhifadhi juzuu 20, mshindi wa kwanza alikuwa Hilal Khamis Hamad (14)
aliyepata sh. milioni 2.5 akifuatiwa na Ally Suleiman Ally (15) aliyepata sh.
milioni 1.3 na mshindi wa tatu alikuwa Salim Khamiis Juma (15) aliyepata sh.
milioni moja.
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
JUMAMOSI,
MEI 26, 2018.
No comments:
Post a Comment