Naibu Waziri Wa Kazi Ajira Na Vijana Mheshimiwa Anthony Mavunde
Akigawa Maziwa Ya Asas Kwa Wanafunzi Waliojitokeza Kwenye Viwanja Vya
Nyerere Square jijini Dodoma Kwenye Kilele Cha Unywaji Wa Maziwa Duniani
Ambapo Kitaifa Imeadhimishwa Mkoani Arusha
Wanafunzi Wa Shule Ya Msingi Nkuhungu Ya jijini Dodoma Wakigawiwa Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD.
Wanafunzi Wa Shule Ya Nkuhungu Wakifurahia Maziwa kutoka ASAS DAIRIES LTD.
Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Na Mkuu Wa
Mkoa Wa Arusha Mh. Mrisho Gambo Wakipokea Maziwa Kutoka Kwa Mwakilishi
Wa Asas Dairies Lipita Mtimila Kwa ajili Ya Shule Za Mkoa wa Arusha
Ambapo ASAS DAIRIES LTD Wametoa Maziwa pakiti 15,000 Kwa Wanafunzi wa
mkoa huo.
Naibu Waziri Wa Tamisemi Mheshimiwa Josphat Kandege Akisaini
Kitabu Cha Wageni Alipotembelea Banda La ASAS DAIRIES LTD Kwenye
Madhimisho Wa Wiki Ya Maziwa Kitaifa yaliyofanyika Mkoani Arusha.
Mheshimiwa Richard Kasesela Akuu wa Wilaya ya Iringa Na
Mkurugenzi Wa ASAS DAIRIES LTD Ahmed Salim Asas wakiwa Kwenye Viwanja
Vya Ngombe Mjini Iringa Kwenye Kilele Cha Madhimisho Ya Wiki Ya Maziwa
Duniani.
Wanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngombe Wakifurahia Maziwa Ya ASAS
DAIRIES LTD wakati Mkuu wa wilaya ya Iringa Bw. Richard Kasesela na
Mkurugenzi wa ASAS DAIRIES LTD Bw. Ahmed Salim Asas walipokuwa
wakiwagawia.
Mheshimiwa Kasesela Akimpatia Maziwa Mmoja wa Mwanafunzi Wa Shule Ya Kihesa Ngome mjini Iringa.
....................................................................................................
ASAS
DAIRIES LTD imegawa zaidi ya pakiti 400,000 kwenye shule mbalimbali za
mikoa ya IRINGA, ARUSHA, MBEYA na DODOMA. wakati wa maadhimisho ya
wiki ya Maziwa duniani ambapo kitaifa inafanyika mkoani Arusha.
ASAS
DAIRIES LTD ilianza kampeni hii Tarehe 22 mwezi wa Tano na kufikia
zaidi ya shule 108 na Wanafunzi 67,000. Hii inatokana na uhamasishaji wa
unywaji wa Maziwa Mashuleni ambao unafanywa na ASAS DAIRIES LTD kila
mwaka.
Katika
kufikia lengo la watanzania kunywa maziwa kwa wingi kampuni ya ASAS
DAIRIES LTD imejikita katika kampeni hiyo ili kuwafanya watoto ambao
watakuwa wazazi wa baadaye kutumia maziwa kwa wingi ili kuimarisha afya
zao pamoja na vizazi vyao kwa siku za baadaye.
Mkurugenzi
wa Kiwanda cha ASAS DAIRIES LTD Bw. Amded Salim Asas amesema huu ni
mwendelezo wa kampeni hiyo na lengo la kampuni hiyo kwa mwakani ni
kuzifikia shule za msingi nchi nzima, Bw. Ahmed Asas ameishukuru
Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli
kwa ngazi zote jinsi ambavyo imekuwa ikitoa ushirikiano kwa kwao na
kuifanya ndoto ya Tanzania ya Viwanda kwenda kutimia kwa mafanikio
makubwa.
No comments:
Post a Comment