Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei, akizungumza katika hafla ya kutoa zawadi kwa washindi wa Kampeni ya Shuhudia Kombe la Dunia na Tembo Card Visa.
Mshindi wa kampeni ya ‘Shuhudia kombe la Dunia na Tembokadi viza’ inayoendeshwa na Benki ya CRDB Tanzania, Emmanuel Mseja (katikati), ambaye ni kipa wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba SC, akipokea zawadi ya runinga na kisimbusi cha DStv wakati wa hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam Juni 1, 2018.
NA MWANDISHI WETU
NA MWANDISHI WETU
MLINDA
mlango wa Klabu ya Soka ya Simba, Emmanuel Mseja ameshinda runinga na
king’amuzi cha DSTV kwenye kampeni ya ‘Shuhudia kombe la Dunia na Tembokadi
viza’ inayoendeshwa na Benki ya CRDB Tanzania.
Ushindi
wa Mseja ulitangazwa Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk.
Charles Kimei alipowakabidhi zawadi washindi wa wiki tatu za mwanzo za kampeni
hiyo.
Akizungumza
kabla ya kugawa zawadi hizo, Dk. Kimei alisema kwa wiki tatu walipatikana
washindi 15 kati yao watatu walishika namba moja kila wiki watakabidhiwa tiketi
kwa ajili ya safari ya Russia kushuhudia kombe la dunia.
“Kila
wiki tulipata washindi watano, waliochanja sana walishika nafasi ya kwanza na
hao watakwenda kushuhudia mechi za ufunguzi za kombe la dunia huko Russia.
“…Safari
ya Russia imelipiwa kila kitu mshindi anatakiwa kwenda kufurahia maisha akiwa
huko,” alisema Dk. Kimei.
Washindi
watatu watakaokwenda Russia kuangalia mechi za kombe la dunia ni Mohamed
Kinjenge, Hemant Josh na Nuru Kisome.
Akizungumzia
ushindi huo Mseja alisema anafurahia huduma za benki hiyo na kwamba hakutegemea
kuwa mshindi licha ya kwamba ni utaratibu wake wa kawaida kuchanja.
“Mimi
huwa nachanja ninapofanya manunuzi mara nyingi sana sikuwa najua kama siku moja
nitashinda namshukuru Mungu na kuwapongeza wlaiobuni shindano hili. Nitaendelea
kuchanja naamini naweza kuipata safari ya Russia,” alisema mlinda mlango huyo
wa mabingwa wa soka Tanzania.
Washindi
wengine waliopata seti ya luninga na kingamuzi cha DSTV ni Zubeda Chande,
Mgullu Mgullu, Mats Idvall, Jenny Correia, Mueen Ibaya, Hassan Mwinyigogo,
Elias Patrik, Anthhony Shayo, John Mwangulangu, Karen Kanza na Wetermack
Batanyita.
Kwa
mujibu wa Dk. Kimei lengo la kampeni hiyo ni kuwajengea wateja wao utamaduni wa
kutumia kazi zao kufanya malipo na manunuzi mtandaoni.
Kampeni
ya shuhudia kombe la dunia na Fifa mwaka 2018 na Tembokadi Visa ilizinduliwa
mwanzoni mwa Aprili kwa benki ya CRDB kushirikiana na Visa International
miongoni mwa wadhamini wa kombe la dunia.
No comments:
Post a Comment