HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 03, 2018

BUJORA DANCE GROUP WAREJEA KWA SHANGWE NCHINI

 Kiongozi wa msafara Hassan Ngoma(katikati) akiwa pamoja na wanakikundi cha Ngoma cha Bujora cha Mkoani  Mwanza wakiwa wamewasili kutoka Nchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti.

Na Agness Francis, Globu ya Jamii

KIKUNDI cha  ngoma cha Bujora Dance  kililokwenda Nchini India katika tamasha la michezo ya asili Afrika kimerejea nchini. 

Kundi hilo lililofanya vizuri zaidi katika mashindano ya Tulia Traditional Dances Festival 2018  ambao waliibuka kuwa ndio washindi limeifanya Tanzania kuwa kivutio huko nchini India.

Ambapo kundi hilo kutokea mwanza Mei 25 mwaka huu ndio lilianza kufanya kazi hiyo ya michezo  asili ya Mtanzania ambapo waliifanya nchi yetu kuwa kivutio katika tamasha la hilo iliyoshirikisha nchi nane  lenye lengo la kuimarisha mahusiano ya kitamaduni.

Kiongozi wa msafara huo Hassan Ngoma amesema kuwa  tamasha hilo lililokonga nyoyo za watu wengi sana  lilifanyika katika miji mitatu  New Delhi, khairagah pamoja na Chandigarh huko nchini India.

Ambapo Usiku wa May 27 heshima nyingine ya Tanzania ilitengenezwa katika mji wa Chandigarh nchini hapo huku kundi  hilo la ngoma za asili  walionyesha tena uwezo wao katika tamasha hilo.

Ngoma amesema usiku wa Mei 30 ndio walihitimisha kufanya maonyesho yao  katika tamasha hilo la wiki ya Afrika ambapo walimalizia kwa kutoa burudani ya uhakika katika mji wa Khairagarh wakiwa ndio waalikwa pekee katika mji huo.

"Imekuwa fursa nzuri kwetu ya kuitangaza tamaduni ya kitanzania kwa nchi mbali mbali lilitoshiriki tamasha la michezo ya asili Afrika" amesema Hassan Ngoma.
Kikundi cha Bujora kikiwa kimewasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam wakitokeaNchini India walipokuwa wameenda kwenye tamasha la ngoma za asili kwa mataifa ya Afrika takribani nane yaliyoanza kutimua vumbi Mei 25 hadi Mei 30 katika miji mitatu tofauti. 

No comments:

Post a Comment

Pages