Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akita ohotuba yake katika hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol katika soko la hisa la Dar es Salaam. Kulia ni Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol, Dk. Gidion Kaunda.
Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol, Dk. Gidion Kaunda, akizungumza katika hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni hiyo katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Meneja Mahusiano wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Charles Shirima (kushoto), akiwa katika hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya, Kikwete, akizungumza katika hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama na kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Jonathan Njau.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, akipiga kengere wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni ya Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, akifafanua jambo wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, akifurahia jambo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Jonathan Njau, akizungumza wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Wageni mbalimbali..
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akiteta jambo na Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya, Kikwete.
Wageni mbalimbali.
Wageni waalikwa.
Baadhi ya wageni waalikwa.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, akitoa hotuba yake.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, akimpongeza Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, baada ya kutoa hotuba yake.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya kuorodheshwa kwa hisa 69, 165,170 za Kampuni Nicol katika Soko la Hisa la Dar es Salaam.
Rais mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete (wa pili kuli), akiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bodi ya Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE), Jonathan Njau (kulia), Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Uwekezaji ya Nicol, Dk. Gidion Kaunda.
Rais mstaafu Dk. Jakaya Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
NA MWANDISHI WETU
RAIS Mstaafu Jakaya Kikwete ameipongeza Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kwa kufanikiwa kuorodhesha hisa 69,165,170 za Kampuni ya Uwekezaji wa pamoja ya National Investment Company Limited (NICOL) katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE).
Itakumbukwa kwamba NICOL iliondolewa katika orodha ya kampuni ya kampuni zilizoorodheshwa DSE Juni 2011 kutokana na matatizo ya kiutendaji katika uwekezaji katika uwekezaji.
Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Kikwete alisema kwamba lengo la kuisajili Nicol ilikuwa ni kuwasaidia wazawa kukua kiuchumi.
"Nakumbuka wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa kuhoji kwanini Nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo," alisema.
Aidha alisema kwamba hakuwahi kuusikia mgogoro wa NICOL wakati wa utawala wake.
"Lengo lilikuwa kusaidia wazawa kujijenga kuichumi na kukuza maendeleo, nimesikia leo hadithi ya Nicol katika uongozi wangu sikusikia kabisa mgogoro wao," alisema Kikwete.
Aidha aliipongeza CMSA kwa utendaji kazi wake, ikiwemo kusimamia kwa madhubuti masoko ya mitaji.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama, alisema kwamba mamlaka iliidhinisha mauzo ya awali ya hisa za Kampuni ya NICOL kwa umma yaani (Initial Public Offers – IPO).
Alisema kwamba mauzo hayo yalifanyika katika awamu mbili, moja ikiwa ni Novemba 2004 ambapo Kampuni NICOL ilifanikiwa kukusanya sh. bilioni 3.9 na awamu nyingine ilifanyika Oktoba mwaka 2007, ambapo jumla ya sh. bilioni 5.6 zilikusanywa.
"Kutokana na mwenendo mzuri wa mauzo ya hisa, Kampuni hii ilifanikiwa kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar Es Salaam Julai 15, 2008. Hata hivyo, kutokana na matatizo ya uongozi na kiutendaji katika uwekezaji,kampuni hii tuliiondoa sokoni Juni mwaka 2011 na CMSA iliamuru kuwasimamishwa kwa Wakurugenzi wa Bodi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya NICOL ili kuwezesha uongozi mpya kuteuliwa na wanahisa wote,"alisema.
Mkama alisema kwamba Aprili 14, 2012, Kampuni ya NICOL ilifanikiwa kupata uongozi mpya chini ya Mwenyekiti wake Dk. Gideon Kaunda na ofisa Mtendaji Adam Kinoni ambao ulithibitishwa kupitia Mkutano mkuu wa wanahisa wote.
"Uongozi huu umeweza kushughulikia matatizo ya uendeshaji wa kampuni na uwekezaji ambayo yalisababisha Kampuni hii kuondolewa katika soko la hisa,NICOL pia imeweza kutekeleza maelekezo yote yaliyokuwa yametolewa na CMSA Mamlaka ili kukidhi hadhi ya kuendelea kuwa kwenye Soko la Hisa.
Mkama aliyataja masharti ambayo CMSA ilitoa kwa NICOL nikutoa notisi kwa wanahisa kuwaelezea kile kinachoendelea ndani ya kampuni na kutayarisha mkutano mkuu wa wanahisa,kuhakikisha mahesabu ya NICOL tokea mwaka 2009 yanakamilishwa kama ilivyopangwa, Kuteua wakaguzi wa nje (External Auditos) kwa ajili ya hesabu za kampuni kwa miaka ya fedha 2010-2015 ili kuhakikisha kuwa mkutano mkuu unafanyika Octoba.
Alisema masharti mengine waliyowapa ni Kutayarisha taarifa ya shughuli za kampuni ikiwemo kuiwezesha kuanza kutekeleza kazi zake na kuangalia uwezekano wa kuirudisha kampuni sokoni.
Mkama alisema NICOL imefanya mabadiliko ikiwa ni pamoja na kuandaa mkakati mpya wa uwekezaji unaohusisha kuugawa uwekezaji wake kwenye dhamana za serikali kwa lengo la kupata anuwai, kuleta ulinzi wa mtaji na uongozi madhubuti.
"Mageuzi makubwa ya kiutendaji na matokeo mazuri ya mwenendo wa Kampuni ya NICOL ni matokeo ya usimamizi madhubuti wa CMSA uliodhihirika katika kusimamia sheria, miongozo na kanuni za masoko ya mitaji. Misingi hiyo ndiyo iliyotumika kuiwakilisha serikali kulinda masilahi ya wawekezaji katika kampuni ya NICOL, na hivyo kukuza thamani ya uwekezaji kutoka sh. 4.6 bilioni Mwaka 2004 mpaka Sh. Bilioni 96.2 mwaka 2017, sawa na ongezeko la asilimia 1,991,"alisema.
Mwenyekiti wa DSE, Jonathan Njau, alisemakwamba DSE wana furaha kuiona Nikol ikirejea tena katika soko la hisa kwaajili ya kuuza, kununua, na kukuza uchumi wa kampuni pamoja na taifa.
Aliwaasa viongozi wa Nicol kufuata taratibu ikiwa wanataka kuendelea kukaa katika soko lazima wafuate sheria na utaratibu ikiwemo kutengeneza mahesabu na kukaguliwa kwa uwazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Nicol, Adam Kinoni, alisema kwamba wazo la kuanzisha Nicol lilianza 1999 ili kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Alisema kwamba yaliyotokea hapo nyuma na wanahisa kwenda mahakamani kuchukua hisa zao ikiwemo Nicol kutofuata utawala bora, uwekezaji wa kiholela hali iliyosababisha kampuni kupata hasara hayatajitokeza tena kwani wamerekebisha mapungufu ikiwemo kuweka hesabu zao sawa.
Alisema kwamba Nicol ilipitia changamoto nyingi ikiwemo kufunguliwa kesi na viongozi waliopita ikiwemo uongozi wa sasa kulazimika kufanya kazi nje ya ofisi kwasababu ya viongozi waliopita kutokubali kuachia.
Alisema kwamba kurudishwa kwa Nicol katika soko la hisa la DSE wenyekiti bodi ya NICOL, Dk. gideon Kaunda, alisema kwamba wamerudi sokoni kwa kasi hivyo itauza, kununua na kuzalisha zaidi.

No comments:
Post a Comment