HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 11, 2018

DK. MNDOLWA AUNGURUMA JIJINI MWANZA, LEO


Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akizungumza na viongozi wa CCM na wa Jumuiya hiyo mkoani Mwanza, katika mkutano uliofanyika katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza, leo. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo na kulia ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza Cornel Magembe na Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanziar Haidar Haji Abdallah.

Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah akizungumza wakati wa mkutano huo.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Erasto Sima akizungumza wakati wa mkutano huo.
Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania, Christina Joram akizungumza, alioopewa nafasi ya kusakimia kwenye kikao hicho.

Baadhi ya viongozi na watumishi wa Jumuiya ya Wazazi wakiwa kwenye kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Dk. Edmund Mndolwa akiagana na Katibu wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mwanza, Adam Soud kabla ya kuondoka Mwanza kwenda mkoani Mara baada ya kikao hicho.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Mwanza Cornel Magembe akimuonyesha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania Edmund Mndolwa kiwanja cha Jumuiya hiyo kilichopo eneo la Nyamagana, Dk. Mndolwa alipokagua kiwanja hicho, akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mwanza, leo. Wapili kusho ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania upande wa Zanzibar Haidar Haji Abdallah na watatu ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo mkoa wa Mwanza Dk. Anthony Diallo. (Picha zote na Bashir Nkoromo).

No comments:

Post a Comment

Pages