MKUUwa
Mkoa wa Mwanza, Bw. John Mongella amesema mafanikio makubwa
yaliyopatikana katika kilimo cha zao la pamba kwa mwaka huu, yametokana
na hamasa iliyotolewa na viongozi wakuu wa Serikali.
Amesema
kwa mwaka huu wanatarajia kupata mavuno makubwa kutoka katika kilimo
cha zao la pamba kwa sababu wakulima wengi wamelima na baadhi tayari
wameshaanza kuvuna.
Bw.
Mongella amesema Rais Dkt. John Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
walitoa maelekezo na ufuatiliaji wa karibu wa kilimo cha mazao makuu
matano ya biashara nchini, likowemo na zao la pamba.
Akizungumza
kuhusu maendeleo ya zao hilo jijini Mwanza leo (Jumanne, Juni 12,
2018), Bw. Mongella amesema zao la pamba litasaidia kufufua viwanda vya
mafuta ya kula, nguo pamoja na kuongeza ajira.
Amesema
baada ya Rais Dkt. Magufuli kuhamasisha kilimo cha zao la pamba,
ambacho kilianza kusuasua nchini, viongozi waliitikia na kuwahimiza
wakulima wachangamkie fursa hiyo, ambao walikubali.
“Tunashukuru
kwa hamasa na miongozo iliyotolewa na viongozi wetu kwa sababu
iliongeza ari kwa wakulima kulima zao la pamba kwa wingi, pia hamasa
hiyo imeongeza muamko kwa wananchi kulima mazao mengine, ilikiwemo la
mpunga,” amesema.
Pia
Bw. Mongella ameishukuru Serikali kwa kuagiza pamba itakayovunwa iuzwe
kupitia minada itakayosimamiwa na Chama cha Msingi cha Ushirika (AMCOS)
katika kila eneo, jambo ambalo limesaidia kufufuka kwa vyama hivyo.
Amesema
wanatarajia kuwahamasisha wakulima wote wa mkoa huo pamoja na wafugaji
na wavuvi wajiunge katika AMCOS zilizoko katika maeneo yao, ili kuweza
kuirahisishia Serikali kufanyanao kazi.
Hata
hivyo, Bw. Mongella ametoa wito kwa wakulima kutumia taasisi za kifedha
kwa ajili ya kuhifadhi fedha zao na wajijengee nidhamu ya matumizi,
ambayo itawapa fursa ya kuwekeza kwenye miradi ya maendeleo.
No comments:
Post a Comment