Kaimu
Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa NMB, Boma Raballa, na Naibu Mkurugenzi wa
Halo Pesa, Vu Tuan Long, wakisaini mkataba wa ushirikiano
utakaowawezesha mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za Kibenki za NMB
kupitia huduma kabambe kwa wakala (Siper-Agent Service) kwa ajili ya
kuweka na kutoa fedha kupitia benki hiyo.
Kaimu
Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa NMB, Boma Raballa, na Naibu Mkurugenzi wa
Halo Pesa, Vu Tuan Long, wakionyesha mkataba wa ushirikiano utakaowawezesha mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za Kibenki za NMB kupitia huduma kabambe kwa wakala (Siper-Agent Service) kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kupitia benki hiyo.
Kaimu
Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa NMB, Boma Raballa, akizungumza katika hafla ya kusaini mkataba
wa ushirikiano wa kibiashara utakaowawezesha mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za
Kibenki za NMB kupitia huduma kabambe kwa wakala (Siper-Agent Service)
kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kupitia benki hiyo.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa hafla fupi ya kusaini makubaliano ya kibiashara na benki ya NMB.
Baadhi ya waandishi wa habari katika hafla hiyo.
Na Costancia Nkindi
KATIKA kutekeleza azma
ya kuboresha utoaji huduma za kifedha kwa wananchi wenye vipato tofauti,
Kampuni ya mawasiliano ya Halotel na Benki ya NMB zimeingia katika ushirikiano utakaowawezesha
mawakala wa Halo Pesa kutumia huduma za Kibenki za NMB kupitia huduma kabambe
kwa wakala (Super-Agent service) kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kupitia
benki hiyo.
Hatua hiyo
itawawezesha mawakala wote wa huduma za kifedha kupitia Halopesa nchi nzima
kuweza kuweka na kutoa pesa taslim
kupitia tawi lolote la benki ya NMB na
kuweza kuwanufaisha mamilioni ya watanzania na huduma za kifedha kwa njia ya
mtandao kwa ukaribu na urahisi zaidi.
Naibu Mkurugenzi wa
Halo Pesa, Vu Tuan Long amesema ushirikiano huo ni hatua nyingine kubwa katika
utoaji wa huduma za kifedha kupitia
mawakala ambapo sasa huduma ya kutoa na kuweka pesa kwa mawakala zitafanyika
kupitia benki ya NMB.
“Huduma za kifedha kwa
njia ya mtandao ni sekta inayokuwa kwa kasi hapa nchini. Ushirikiano huu
utawawezesha mawakala wa Halo Pesa kuweza kupata huduma ya kuweka na kutoa pesa
kiurahisi kupitia matawi yote ya NMB
nchi nzima,” alisema Long.
Alisema hadi sasa hivi Halotel ina mawakala zaidi ya
55,000 walioenea nchi nzima. Mawakala wa Halo Pesa watatumia namba za USSD za
Halo Pesa ambazo ni (*150*88#) kwa kutoa
fedha katika benki ya NMB pamoja na kutoa pesa
kwa fomu maalum za kuweka fedha wakiwa katika matawi ya benki hiyo.
Kwa upande wake Kaimu
Mkuu wa wateja wa kati na wadogo wa NMB, Boma Raballa alisema benki hiyo
imekuwa ya kwanza katika kutoa huduma zenye ubunifu ambazo zinalenga kutatua
changamoto mbalimbali ndani ya jamii, “Tulitambua kuna uhitaji katika upatikanaji wa fedha kwa
mawakala” alisema Raballa.
“Mtandao mkubwa wa
matawi yetu unaoenda sambamba na kaulimbiu yetu ya “Karibu nawe” imekuwa sehemu
kubwa ya mafanikio katika utoaji wa
huduma za kifedha. Hadi sasa tuna matawi zaidi ya 220 ambayo yako zaidi ya
asilimia 98 ya wilaya za nchi hii zitarahisisha sana upatikanaji wa huduma kwa
mawakala”. Alisema Raballa.
Tanzania ni miongoni
mwa nchi zinazoripotiwa kuwa na watumiaji wengi wa huduma za kifedha wakifikia
takribani milioni 19, hivyo uhitaji na upatikanaji wa fedha kwa watumiaji hao
imekuwa ni changamoto kubwa kwa baadhi ya watumiaji, kupitia benki ya NMB sasa
mawakala na watoa huduma za kifedha sasa watakuwa na nafasi ya kupata huduma
karibu yao.
No comments:
Post a Comment