Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na
Ajira ,Anthony Mavunde akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga washiriki 70 wa Programu ya
Kili Challenge 20018 wanaopanda Mlima Kilimanjaro kwa lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya vita dhidi ya Virusi vya Ukimwi na Ukimwi.
Baadhi ya washiriki wa Changamoto hiyo pamoja na wageni mbalimbali wakifuatilia hotuba zilizokuwa wakati wa Hafla hiyo iliyofanyika lango la Machame .
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maswala ya UKIMWI,Oscer Mukasa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Mwakilsihi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tanapa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witnes Shoo (kushoto) akiwa na Mkuu wa wilaya ya Hai,Onesmo Buswelu pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Mlima Kilimanjaro,Betrita Loibook wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Tume ya taifa ya kudhibiti UKIMWI Tanzania ,Leonard Maboko akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga washiriki 70 wa changamoto ya kupanda mlima Kilimanjaro kwa ajili ya kuchangisha fedha za mapambano dhidi ya UKIMWI ,zoezi hilo linaratibiwa na Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM).
Makamu wa Rais wa Kampuni ya kuchimba Dhahabu ya Geita (GGM) Simon Shayo akizungumza wakati wa kuwaaga washiriki 70 wa changamoto hiyo ya kupanda mlima Kilimanjaro na kuuzunguka kwa kutumia Baiskeli.
Mgeni Rasmi katika tukio hilo, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na
Ajira ,Anthony Mavunde akikabidhi Bendera kwa washiriki wa changamoto hiyo kwa njia ya kuzunguka mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baiskeli.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na
Ajira ,Anthony Mavundeakijaribu kuendesha Baiskeli kuashiria uzinduzi wa Changamoto ya kuzunguka Mlima Kilimanjaro kwa kutumia Baikeli.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na
Ajira ,Anthony Mavundeakishirikia zoezi la Kupanda Mlima Kilimanjaro kuashiria mwanzo wa safari ya wapandaji 40 wanashiriki zoezi hilo.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro,Hamis Issah ni miongoni mwa washiriki walioanzisha safari hiyo.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witnes Shoo (kulia) akiwa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro Betrita Loibook (Kushoto) pia wameshiriki katika kuanzisha safari ya wapanda Mlima hao.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini
ZAIDI ya Sh Bilioni 20 zimekusanywa
kutoka kwa mashirika 40 yasiyo ya kiserikali pamoja na taasisi mbalimbali za
serikali kwa ajili ya kusaidia katika kampeni za kupambana dhidi ya Virusi vya
Ukimwi na Ukimwi ambapo tayari Mamilioni ya watanzania wamekwisha nufaika nazo.
Fedha hizo zimekusanywa kampuni ya
Kuchimba dhahabu ya Geita (GGM) kupitia changamoto ya kupanda Mlima
Kilimanjaro, ijulikanayo kama “Kili Challenge” tangu mwaka 2001 ilipoanzishwa
,mwaka huu ukiwa mwaka wa 17 ikishirikisha washiriki 70 watakao shiriki kupanda
Mlima huku wengine wakizunguka mlima huo kwa kutumia Baiskeli .
Akizungumza wakati wa Hafla ya kuwaaga
washiriki wa Programu ya Kili Challenge 20018 iliyofanyika katika lango la
kupanda Mlima Kilimanjaro la Machame ,Makamu wa Rais wa GGM, Simon Shayo
amesema Progaramu hiyo imepanua wigo wa kusaidia Taasisi zinazojikita kuhudumia
wachimbaji wadogo wadogo pamoja na maeneo ya wavuvi ambako tafiti zinaonyesha
wako kwenye mazingira hatarishi ya kuambukizwa VVU.
“Kila siku na kila mwaka ,tukio hili la hisani linaendelea kuwa na
matokeo makubwa kwa jamii inayotuzunguka ,ninayo furaha leo kutagaza kwamba
kupitia Kili Challenge tumeweza kuchangisha zaidi ya Bilioni 20 .”alisema
Shayo.
Alisema
fedha hizo zimekusanywa kutoka katika Mashirika 40 yasiyo ya kiserikali
(N.G.O,S) pamoja na taasisi mbalimbali za serikali kupitia Tume ya taifa ya
kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo watanzania zaidi ya Milioni moja wamenufaika
nayo.
Shayo alisema mbali na tukio
hilo ,KAmpuni ya GGM imeendelea kuwekeza katika miradi ya kijamii ikiwemo ya
Elimu,Afya,Maji na miundombinu ya barabara katika mkoa wa Geita na kwamba
imetenga kiasi cha Sh Bil 9.2 kwa ajili ya huduma za jamii nah ii ni baada ya
kuingia makubaliano na Wilaya ya Geita pamoja na Halmashauri yake.
Mgeni rasmi katika tukio hilo ,Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana na Ajira ,Anthony Mavunde amesema
Serikali ya Tanzania inajivunia jitihada hizi ambazo zinaonekana kuwa endelevu
katika utafutaji wa raslimali za udhibiti wa UKIMWI nchini.
“Kama nilivyosema TACAIDS imekuwa
ikishirikiana kwa karibu na GGM kuhakikisha jambo hili linatekelezwa kwa
tafsiri ya kuoanisha Changamoto za mapambano dhidi ya UKIMWI na ugumu wa
upandaji wa Mlima Kilimanjaro kupitia njia ngumu ya Machame na uzungukaji wa
Mlima Kilimanjaro kwa baiskeli.”alisema
Mavunde.
Hadi sasa zaidi ya Watu 700 kutoka
duniani kote wameshiriki katika changamoto hiyo ya kihistoria ya upandaji Mlima
kupitia programu ya “Kili Challenge” na kukusanya fedha ambazo zimesaidia
maeneo mbalimbali yakiwemo makundi ya Wajane, Watu Wanaoishi na Virusi vya
UKIMWI, Watoto yatima, Vijana, pamoja na Taasisi zinazotoa huduma muhimu za
UKIMWI.
Aidha, Fedha hizi zimetumika
kuboresha huduma za Hospitali mbalimbali nchini zikiwemo za Mkoa wa Geita na
Kibong’oto Mkoani hapa na ujenzi wa Vituo vinne (4) vya maarifa kwenye njia kuu
za usafirishaji.
No comments:
Post a Comment