Katibu wa
Rais, Ngusa Samike, akimkabidhi Rehema Kadogosa ambaye ni Mama wa Mtoto Latifa
Kadogosa (13) aliyelala kitandani kiasi cha Shilingi milioni tano (5,000,000/-)
fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt.
John Pombe Magufuli kwa ajili ya kumsaidia mtoto huyo ambaye ana matatizo ya
kiafya jijini Dar es Salaam.
Katibu wa
Rais Ngusa Samike akimuangalia mtoto huyo
Latifa Kadogosa(13) ambaye amepakatwa na Mama yake Rehema Kadogosa
Mwenge jijini Dar es Salaam.
Meneja wa
Tawi la Benki ya CRDB Mikocheni, Rehema Moyo, akimkabidhi Kadi ya Benki, Rehema
Kadogosa, mama mzazi wa Latifa Kadogosa mara baada ya kufungua Akaunti katika
tawi hilo kwa ajili ya kutunza fedha hizo alizopewa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli pamoja na fedha nyingine atakazosaidiwa na wadau wengine. PICHA NA IKULU.
No comments:
Post a Comment