Wafanya
biashara katika soko la Ferry jijini Dar es Salaam wameomba mamlaka za serikali
kutoa elimu ya kuuzu kutunza mazingira ya Bahari ili kuendana na mabadiliko ya
hali ya hewa. Kwa kufanya hivyo, Wananchi waofanya shughuli zao za kila
wataweza kupata uelewa na kua chachu ya kutunza mazingira jambo ambalo litaweza
kuongeza upatikanaji wa samaki na pia kuweka fukwe za Bahari katika mazingira
safi muda wote.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini
Dar es Salaam jana, mfanya biashara wa samaki katika soko la Ferry Said Idd
alisema kuwa amekuwa kwenye shunguli za kuuza na kuvua samaki kwenye soko hilo
kwa zaidi ya miaka kumi na kwa siku za hivi karibuni ameshuhudia upungufu wa
hupatikani wa samaki kama ilivyokuwa miaka ya nyuma na pia kuendelea kuchafuka
kwa fukwe za Bahari.
Said alisema hayo wakati wa futari
iliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Kivukoni Henry Sato Massaba kwa wafanya
biashara wa kati hiyo ambayo wengi wao ni wafanya biashara kati ya soko la
Ferry. Diwani Massaba pia ndiye mwenyekiti wa bodi wa soko hilo.
‘Naomba kutoa wito wangu kwa serikali kutoa
elimu kuhusu utanzaji safi wa mazingira na sana sana usafi wa fukwe za Bahari.
Kama viumbe hai, samaki nao wanahitaji kuishi kwenye sehemu salama. Natoa mfano
mzuri tu, siku za nyuma kulikuwa na uvuvi haramu hapa. Lakini serikali iliona
hilo kama changamoto na ikaweka nguvu na mpaka sasa uvuvi haramu umeisha. Kwa
kufanya hivi serikali inaweza kutoa elimu na sisi kwa kushirikiana tunaweza
kuweka mazingira yetu yakawa safi na pia salama kwani hapa pia kuna biashara za
mama lishe ambazo zinatakiwa kufanywa kwenye sehemu salama, alisema Said.
Kwa sasa upatikani wa samaki ni wa tabu
sana. Kuna muda wavuvi wanakaa Bahari kwa zaidi ya siku tatu. Wengine
wanalazimika kwenda mpaka Mafia kufuata samaki. Zamani hayo mambo hayakuwepo na
ukiangalia utaona uchafu wa mazingira umechangia, aliongeza Said.
Kwa upande wake, Diwani Massaba alisema
kuwa Kata yake imekuwa ikiendesha operesheni za mara kwa mara za kutunza
mazingira na hasa kwenye fukwe za Bahari. Unajua hapa soko la samaki la Ferry
ni la kiwango cha Kimataifa. Tunapokea wageni na wateja wengi wa kila aina. Ni
muhimu kwetu sote kutunza mazingira, alisema Massaba.
Kuhusu kuandaa futari kwa wafanya biashara,
Diwani Massaba alisema ‘Huu ni utamanduni kwa watangulizi wangu kuandaa futari
angalau mara moja kila inapofika mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Kwa kukaa pamoja na
kupata futari inaonyesha upendo na mshikamano. Vile vile, inatoa nafasi kwa sisi
wafanya biashara na wakazi wa Kata ya Kivukoni kukaa pamoja na kujadaliana
Maendeleo yetu ya kata. Wakazi wetu wamekuwa na mchango kwenye miradi ya
Maendeleo na natoa wito tuendelee hivi hivi kwani Maendeleo ni yetu wote,
aliongeza Diwani Massa
No comments:
Post a Comment