Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL),
imekamilisha uteuzi wa wachezaji 3 watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/2018.
Wachezaji
watatu waliobaki katika kinyang'anyiro hicho ni Emmanuel Okwi, John
Bocco na Erasto Nyoni wote wa Simba, ambapo kamati ya Tuzo hiyo ya
Mchezaji Bora imeandaa utaratibu wa kupiga kura kuwashirikisha Wahariri
wa Habari za Michezo, manahodha wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom na
makocha wa timu za Ligi Kuu.
Pia
kamati imekamilisha uteuzi wa wachezaji watakaowania tuzo katika
kategori mbalimbali kwenye sherehe hizo za Tuzo ya Mchezaji Bora wa VPL
itakayofanyika ukumbi wa Mlimani, City Dares Salaam Juni 23 mwaka huu.
Tuzo
16 zinatarajiwa kutolewa siku hiyo, ambapo baadhi ni za kikanuni za
Ligi Kuu Tanzania Bara, ambazo tayari washindi wake wamefahamika, ambazo
ni bingwa, mshindi wa pili, mshindi wa tatu, mshindi wa nne na mfungaji
bora.Ukiacha hizo tano za kikanuni, zipo tuzo 10 ambazo zimefanyiwa
kazi na Kamati ya Tuzo kulingana na takwimu mbalimbali za ligi hiyo,
ambapo tuzo moja nyingine ya Mchezaji Bora chini ya umri wa miaka 20
(Tuzo ya Ismail Khalfan), inayohusisha vikosi vya vijana vya timu za
Ligi Kuu yenyewe inaendelea kufanyiwa kazi kwa vile mashindano
yanaendelea mkoani Dodoma na itakapokamilika watatangazwa wateule
watatu.
Tuzo nyingine
zitakazotolewa siku hiyo ni Timu yenye Nidhamu inayowaniwa na Kagera
Sugar, Simba na Mtibwa Sugar, wakati Mchezaji Bora Chipukizi inawaniwa
na Shaaban Idd Chilunda, Yahya Zayd (Azam) na Habibu Kiyombo (Mbao).
Mwamuzi
Msaidizi Bora inawaniwa na Helen Mduma, Mohammed Mkono na Ferdinand
Chacha, wakati Mwamuzi Bora wateule ni Elly Sasii, Jonesia Rukyaa na
Hans Mabena.
Tuzo ya Kipa
Bora wanaowania ni Aron Kalambo (Prisons), Aishi Manula (Simba) na
Razack Abalora (Azam), huku Kocha Bora wateule ni Abdallah Mohamed
(Prisons), Zuberi Katwila (Mtibwa) na Pierre Lechantre (Simba).
Goli Bora ni Seif Karihe (Lipuli) na Shaaban Idd Chilunda (Azam) ambaye ameingiza mabao mawili.
Tuzo
nyingine ambazo zitatolewa Juni 23 ni Mchezaji wa Heshima ambayo licha
ya kuwa kamati ina majina ya wachezaji mbalimbali inaoona wanastahili
tuzo kwa mwaka husika, lakini haitangazi majina hayo, isipokuwa hutaja
jina la aliyepewa tuzo siku ya sherehe.
Shirikisho
la Mpira wa Miguu Barani Africa CAF limetaja waamuzi kutoka nchini
Somalia kuchezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya makundi kati
ya Gor Mahia ya Kenya na Young Africans ya Tanzania utakaochezwa Uwanja
wa Moi Kasarani Julai 18,2018.
Kwenye
mchezo huo Mwamuzi wa katikati atakua Hassan Mohamed Hagi akisaidiwa na
Mwamuzi namba 1 Hamza Hagi Abdi, Mwamuzi msaidizi namba 2 Suleiman
Bashir Sh.Abdi na Mwamuzi wa akiba Nur Muhidin Mohamed.
Mtathmini
waamuzi anatokea Gabon Jan Olivier Mbera na Kamishna wa mchezo anatokea
Africa Kusini Simphiwe Brian Xaba sambamba na mratibu wa mchezo huo
Nomsa Jacobeth Mahlangu.
Aidha
mchezo wa marudiano kwa timu hizo utakaochezwa July 29,2018 Kwenye
Uwanja wa Taifa wenyewe utachezeshwa na Waamuzi kutoka Mauritius.
Mwamuzi
wa katikati atakuwa Ahmed Imtehaz Heeralall akisaidiwa na Mwamuzi
msaidizi namba 1 Cauvelet Louis Ralph Fabian,Mwamuzi msaidizi namba 2
Akhtar Nawaz Rossaye na Mwamuzi wa akiba Ganesh Chutooree.
Kamishna
wa mchezo anatokea Zambia Patrick Kangwa, Mtathmini waamuzi anatokea
Congo Louzaye Rene Daniel wakati Mratibu anatokea Nigeria Nasiru
Sarkintudu Jibril.
No comments:
Post a Comment