Na Mwandishi Wetu
AZANIA Benki
inajivunia uzalishaji wa huduma kwa kila mmoja kwa wateja wake bila kujali
dini, kabila na jinsia kwa faida na hasara kwa kuandaa futari pamoja na waislamu
walioungana na wateja wa benki hiyo.
Akizungumza juzi
katika hafla ya futari iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Benki hiyo,
Rhimo Nyansaho alisema wameungana na waislam katika futari hiyo ikiwa ni sehemu
yao ya kushirikiana na jamii.
Nyansaho alisema benki
hiyo inasonga mbele kwa sababu ya michango ya jamii katika benki hiyo ndio
maana kipindi cha mfungo wakaona ni sahihi kurudisha pato hilo kwa kufuturu na
jamii yenye uhitaji kama watoto yatima na wengineo.
Mkurugenzi huyo alitumia
fursa hiyo kuisifia benki yake kwamba wanatoa huduma bora na ndio maana faida
inayoongezeka wanairudisha kwa jamii.
Aliipongeza serikali
kwa kuweka mazingira ya kushuka kwa riba katika benki mbalimbali ingawa wao
walishashusha riba zao muda mrefu.
Mwakilishi wa wateja
wa benki hiyo, Deogratius Kifumani aliipongeza benki hiyo kwa huduma zake
inazotoa na kutoa wito kwa jamii kuelekeza mikakati yao ya kiuchumi huko.
Kifumani alisema ubora
wa huduma zao ndio maana inafanikisha matukio muhimu kama hayo katika jamii kwa
kurudisha sehemu ya pato lao.
Sheikh Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo Maulid Kidebe alisema kilichofanywa na benki ya Azania kina maana
kubwa kwa jamii, tukio hilo ni thawabu kubwa zinapatikana kwa sababu
imewakumbuka yatima ambao wanatakiwa kuwa karibu zaidi na jamii.
Sheikh Kidebe alitoa
wito kwa benki na taasisi nyingine kuiga mfano uliofanywa na Azania ili
kusaidia jamii katika mahitaji muhimu.
Mtoto yatima aliyekuwepo
katika futari hiyo, Safina Muhsin aliishukuru na kuiomba benki hiyo kuendelea
kuwa karibu nao kwa masuala mbalimbali.
Katika hafla hiyo ya
futari iliyoandaliwa na benki ya Azania iliwahusisha watoto wa kituo cha Yatima
cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto wa wanaolelewa katika Kituo cha Yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam wakiswali kabla ya kujumuika na wateja wa Azania Bank katika futari.
Sheikh wa Wilaya ya Ubungo, Shjeikh Maulid Kidebe. akiwaongoza wateja wa Azania Bank wakati wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyowahusisha watoto wa kituo cha watoto yatima cha Ijango zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa Azania Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwahusisha watoto wa kituo cha yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wateja wa Azania Bank wakipata futari iliyoandaliwa na benki hiyo na kuwahusisha watoto wa kituo cha yatima cha Ijango Zaidia cha Sinza jijini Dar es Salaam.
Watoto wakipata futari.
Wateja wakipata futari.
Watu mbalimbali wakipata futari.
Baadhi ya wafanyakazi wa Azania Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakipata futari.
Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Ijango Zaidia wakipata futari.
Baadhi ya Watoto Yatima wanaolelewa na Kituo cha Ijango Zaidia wakipata futari.
Watoto wa kituo cha Yatima cha Ijango Zaidia wakisoma duwa.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Azania Bank, Othman Jibrea, akizunguma katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Mteja wa Azania Bank, Deogratius Kufumani, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wateja wa benki hiyo.
Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Azania Bank,
Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Azania Bank,
Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha
watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Azania Bank,
Rhimo Nyansaho, akitoa hotuba yake wakati wa hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake na kuwahusisha
watoto yatima wa kituo cha Ijango Zaidia cha Sinza.
Sheikh Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo Maulid Kidebe, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Azania Bank kwa ajili ya wateja wake pamoja na watoto yatima.
Mkurugenzi wa
Maendeleo ya Biashara wa Azania Bank,
Rhimo Nyansaho, akizungumza na baadhi ya wateja wa benki hiyo.
No comments:
Post a Comment