Na Hamza Temba-Geita
.............................. ............................
Kampuni
ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa madini
ya dhahabu katika eneo la Luahika ndani ya Pori la Akiba
Moyowosi/Kigosi imetakiwa kuondoa vifaa na mitambo yake katika eneo la
hilo ndani ya siku saba kwa amri ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk.
Hamisi Kigwangalla.
Dk.
Kigwangalla ameiagiza Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA
kutoa ilani ya siku saba kwa kampuni hiyo iondoe vifaa na mitambo yake
katika eneo hilo na endapo muda huo utapita bila kufanya hivyo mali hizo
zitataifishwa na kuwa mali ya Serikali kwa kuwa wao ni wavamizi kwa
mujibu wa sheria.
Waziri
Kigwangalla ametoa agizo hilo juzi alipotembelea pori hilo katika
wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo alihitimisha ziara yake ya siku 25
aliyoipa jina la Pori Kwa Pori kwa ajili ya kukagua shughuli za
uhifadhi nchini na kutatua changomoto zake.
Alisema
uwepo wa vifaa na mitambo ya muwekezaji huyo ndani ya hifadhi hiyo
imekuwa kishawishi kikubwa kwa wachimbaji wadogo wa madini kuvamia
maeneo hayo wakiamini kuwa eneo hilo lina dhahabu na kwamba bado
linaruhusiwa kwa shughuli za uchimbaji.
Awali
Meneja wa Pori hilo, Benjamin Kijika alisema kampuni hiyo ilipewa
kibali na Wizara ya Malisili na Utalii kwa ajili ya kufanya utafiti wa
madini ya dhahabu katika eneo hilo kwa mwaka 2005 hadi 2010 na
kuongezewa muda hadi 2012.
Alisema
wakati kibali hicho kinatolewa Sheria ya Uhifadhi wa Wanyamapori namba 5
ya mwaka 2009 ambayo inazuia tafiti kama hizo na shughuli nyingine za
kibinaadamu kwenye maeneo ya hifadhi ilikua bado haijatoka.
Alisema
baada ya hapo wizara haikutoa tena kibali kwa kampuni hiyo licha ya
wizara ya madini kuipa kibali cha kuchimba dhahabu katika eneo hilo
mwaka 2013. Aliongeza kuwa kwa nyakati tofauti Wizara ya Maliasili
imeitaka kampuni hiyo iondoe mali zake zote ndani ya eneo hilo, agizo
ambalo bado halijatekelezwa mpaka sasa.
Kwa
upande wake aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukombe, Josephat Paulo Maganga
alisema atasimamia utekelezaji agizo hilo la Waziri Kigwangalla ili
eneo hilo liendelee kuhifadhiwa kwa mujibu wa sheria.
Alisema
hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto kubwa ya uvamizi wa mara kwa
mara wa wachimbaji wadogo wa madini ya dhahabu hususan katika eneo la
Kigosi Kaskazini na hivyo kupelekea uharibu mkubwa wa mazingira katika
hifadhi hiyo.
Alisema
ili kukabiliana na changamoto hiyo pori hilo limeanzisha kambi mbili za
ulinzi katika eneo hilo kwa ajili ya kudhibiti uharibifu huo ambapo
mpaka sasa kesi 24 zenye wachimbaji haramu 52 zimeshafikishwa mahakamani
huku kukiwa na vielelezo kadhaa ambavyo ni pamoja na baiskeli 102,
viroba vya mchanga unaosadikika kuwa na madini ya dhahabu na vifaa vya
uchimbaji.
Pori
la Akiba Moyowosi/Kigosi ni muunganiko wa mapori mawili yenye ukubwa wa
kilometa za mraba 21,060. Pori la Moyowosi lipo katika wilaya za
Kibondo na Kakonko (Kigoma) na Pori la Kigosi katika wilaya ya
Biharamulo (Kagera), Bukombe na Mbogwe (Geita), Kahama (Shinyanga) na
Kaliua (Tabora).
Pori
hili lina umuhimu mkubwa kiikolojia na kiuchumi kwakuwa pia ni ardhi
oevu ambayo ni chanzo kikubwa cha maji ya ziwa Nyamagoma na Sagara
ambayo huingiza maji mto Malagarasi na hatimaye ziwa Tanganyika, maji
hayo hutumika kwa matumizi mbalimbali ya majumbani na kilimo. Pia
hifadhi hiyo ni makazi muhimu ya wanyamapori adimu kama Nzohe ambao
huliingizia Taifa fedha za kigeni.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akimuagiza Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania TAWA,
Mabula Misungwi (Kulia) kutoa ilani ya siku 7 kwa kampuni ya uchimbaji
madini ya Tanzam 2000 ili itoe mali zake zote katika eneo la Pori la
Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi katika wilaya ya
Bukombe mkoani Geita na endapo muda huo utapita zitaifishwe kuwa mali na
Serikali.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo
ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika
ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi
katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya
siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi
zitaifishwe kuwa mali ya Serikali, Nyuma yake ni Meneja wa Pori hilo,
Benjamin Kijika.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akikagua vifaa na mitambo
ya kampuni ya uchimbaji madini ya Tanzam 2000 katika eneo la Luahika
ndani ya Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi alipotembelea pori hilo juzi
katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe ilani ya
siku 7 kwa kampuni hiyo iondoe mali zake zote na endapo itakaidi
zitaifishwe kuwa mali ya Serikali, Kulia ni Meneja wa Pori hilo,
Benjamin Kijika.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla akioneshwa vielelezo
(mchanga wa madini ya dhahabu na baiskeli) walivyokamatwa navyo
wachimbaji wadogo wa madini katika eneo Pori la Akiba Moyowosi/Kigosi na
Meneja wa Sekta ya Kigosi Kaskazini, Salum Kulunge alipotembelea pori
hilo juzi katika wilaya ya Bukombe mkoani Geita ambapo amegiza itolewe
ilani ya siku 7 kwa kampuni ya Tanzam 2000 iliyokuwa ikifanya utafiti wa
madini ya dhahabu ndani ya pori hilo iondoe mali zake zote na endapo
itakaidi zitaifishwe kuwa mali ya Serikali.
No comments:
Post a Comment