*Asema lengo ni kudhibiti uingizwaji wa silaha haramu nchini
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwaamesema
ukaguzi wa watu na mizigo unaofanywa kwenye kizuizi cha Uvinza mkoani
Kigoma utaendelea kufanyika ili kudhibiti wimbi la uingizwaji wa silaha
haramu nchini.
“Lazima
ukaguzi ufanyuke ili kujiridhisha kama watu wote wanaoingia nchini
wamepita kihalali na kama hawapitishi silaha haramu na vitu vingine
ambavyo haviruhusiwi kuingizwa nchini,”.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumapili, Julai 29, 2018) wakati akizungumza
na wananchi wa wilaya ya Uvinza akiwa katika siku ya pili ya ziara yake
ya kikazi mkoani Kigoma.
Ametoa
ufafanuzi huo baada ya Mbunge wa jimbo la Kigoma Kusini, Bibi Hasna
Mwilima kudai kuwa wananchi wengi wanapata usumbufu mkubwa kutokana na
ukaguzi unaofanywa na Maafisa wa Uhamiaji katika kizuizi cha Uvinza.
Waziri
Mkuu amesema iwapo viongozi wa mkoa huo hawatakuwa makini katika
kufanya ukaguzi kwenye vizuizi watasababisha watu wengi kuingia kiholela
nchini na hivyo kuathiri mipango ya Serikali ya kuwahudumia wananchi
wake.
Wakati huo huo,Waziri
Mkuu amemuagiza Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Brigedia Jenerali Mstaafu
Emanuel Maganga kufuatilia kwa umakini mwenendo wa utendaji kazi katika
kizuizi cha Uvinza.
Waziri
Mkuu amesema iwapo atabaini kuwepo kwa Maafisa wa kizuizi hicho
wanaojiashishughulisha na vitendo vya rushwa pamoja na kuwasumbua
wananchi na abiria wanaopita kizuizini hapo awachukulie mara moja.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMAPILI, JULAI 29, 2018.
No comments:
Post a Comment