Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, ACP, Hamis Issah, akitembelea Kituo Kikuu cha Mabasi mjini Moshi kwa ajili ya ukaguzi wa Magari ya Abiria.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (ACP), Hamis Issah akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Operesheni wa kikosi cha Usalama Barabarani,Mkaguzi ,Peter Mizambwa wakati wa ukaguzi huo uliofanyika katika kituo kikuu cha Mabasi mjini Moshi.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Kilimanjaro, Inp Peter Mizambwa, akimuonesha kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro, ACP, Hamis Issah, moja ya karatasi ambazo zinatumiwa na madereva kama Leseni.
Mkuu wa Operesheni wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa
Kilimanjaro, Inp Peter Mizambwa akimuonesha Kamanda wa Polisi Mkoa wa
Kilimanjaro, ACP, Hamis Issah, alama za leseni ambayo ni halisi .
Kamanda wa Polisi akimuuliza mmoja wa madereva waliokamatwa, matumizi ya silaha ya kisu kilichokutwa katika gari lake.
Mmoja wa Madereva akipelekwa kituo cha Polisi mara baada ya kubainika kutumia leseni ya ndugu yake kuendesha gari.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini
UKAGUZI wa Magari ya Abiria pamoja na Leseni unaofanywa na
Jeshi la Polisi mkoa wa Kilimanjaro
umebaini udanganyifu mkubwa unaofanywa na baadhi ya Madereva wa Magari ya
abiria ukiwemo kuendesha bila Leseni
,Umri wa kuendesha gari kupitiliza ,
wengine wakitumia Leseni za Ndugu zao.
Katika kituo Kikuu cha Mabasi ya abiria yaendayo mikoani na
yale yanayofanya safari zake ndani ya mkoa wa Kilimanjaro,Kamanda wa Polisi
mkoa wa Kilimanjaro Hamisi Issah akiwa ameongozana na Mkuu Operesheni kikosi cha usalama Barabarani
,Peter Mizambwa na maofisa wengine wa Polisi wamefanya ukaguzi.
Katika ukaguzi huo magari zaidi ya 800 yamekaguliwa na
yaliyobainika kuwa mabovu yalizuiliwa kuendelea na safari huku baadhi ya Madereva wakikutwa na silaha katika magari yao vikiwemo
Visu,kamanda Issah akatoa onyo kwa madereva kutembea na silaha pamoja na kujaza
abiria hali inayochangia abiria kukaa katika mikao isiyo rafiki .
Mkuu wa operesheni wa kikosi cha usalama barabarani ,Mkaguzi
wa Polisi Peter Mizambwa akazungumzia Operesheni Nyakua iliyoanza kwa lengo la
kupunguza ajali huku baadhi ya Madereva
na wananchi wakipongeza utaratibu huo.
No comments:
Post a Comment