NA LUSUNGU HELELA, RUVUMA
Katika hali isiyokuwa ya kawaida
Wakazi wa Kijiji cha Ndondo Kata ya Jangwani wilayani Nyasa mkoani Ruvuma wamekiri mbele ya Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga kuwa wamevamia na wanaishi ndani ya eneo la hifadhi
ya pori la akiba la Lipalamba lakini kwa kuwa hilo eneo wameshalizoea wanaiomba serikali kubadilishana nao na
eneo jingine la kijiji lenye ukubwa sawa na eneo hilo walioingia ndani ya
hifadhi hiyo.
Wananchi hao wametoa maombi hayo
jana kwenye kwenye mkutano wa hadhara wa
Naibu Waziri huyo alioambatana na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya
Nyasa kwa ajili ya kuzungumza na wananchi wa kijiji hicho kwenye ziara ya siku
tatu ambayo Naibu Waziri huyo aliifanya ikiwa ni muendelezo wa utekelezaji wa
ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Akizungumza kwa niaba ya
wanakijiji wenzake, Pancrease Ndunguru alisema kuwa mpaka unaotenganisha kati
ya kijiji na pori hilo ni mto unaojulikana kwa jina Tanginyama
lakini wao wamejikuta wamevamia eneo hilo kwa kuanzisha makazi hivyo
wanaomba hiyo sehemu waendelee kuishi lakini
wakubali kubadilishana.
‘’Hili eneo sisi tushalizoea
tunaiomba serikali ikubali ombi letu la kuweza kubadilishana na eneo lingine nje
ya ukubwa sawa na eneo hili Alisema Pancreance Ndunguru.
Naye, Diwani wa
eneo hilo Ditram Nchimbi alimsihi Naibu Waziri alifanyie kazi ombi hilo la wanakijii kwa vile wameonesha uungwana kwa kutambua kuwa
wamevamia baadhi ya eneo katika hifadhi ya Lipalamba lakini kitendo cha kukiri kosa ni uungwana wa hali ya juu hivyo
walifanyie kazi ombi lao.
Akizungumza kwenye mkutano huo,
Naibu waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet Hasunga aliwaambia wakazi wa eneo
hilo kuwa amelisikia ombi lao lakini hata hivyo suala la kubadilishana maeneo
hayo na linaweza likawa sio rahisi kiasi hicho kwa vile sehemu hiyo
kuna wanyama adimu aina ya palahala ambao hawawezi kuhamishika.
Aidha Naibu Waziri huyo aliongeza
kuwa eneo wanalotaka wabadilishane halijajulikana lina ukubwa kiasi gani na eneo
wanalotaka kupewa lina ukubwa kiasi gani.
Kufuatia ombi hilo, Naibu Waziri
huyo alisema kuwa watatuma wataalamu wenye ujuzi wa ikolojia ili kuja kutafiti ya maeneo hayo
baaada ya ripoti hiyo ya wataalamu kukamilika ndipo maamuzi yataweza kufanyika.
Aidha, aliongeza kuwa kwa kuwa
Wizara ya ardhi ndio wenye dhamana ya kusoma ramani, hivyo wataiomba Wizara
hiyo iweze kutuma watalamu kwa ajili ya kusoma ramani
Katika hatua nyingine Naibu
Waziri huyo alipiga marufuku kwa mwanakijiji yeyote kuingia katika eneo hilo
lenye mgogoro kati ya wananchi na serikali kwa ajili ya kufanya shughuli za
kilimo mpaka pale maamuzi yatakapofanyikiwa.
Pori la akiba la Lipalamba linalomilikiwa
na Mamlaka ya Wanyamapori Tanzania TAWA ina ukubwa na ni hifadhi mpya yenye
ukubwa wa kilomita za mraba liko mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.
Awali Mkuu wilaya hiyo, Elizabeth
Chilambo aliwataka wananchi hao kuwa
mstari wa mbele kwa kuwafichua wanakijiji wenzao wanaojihusisha na ujangili na vitendo vya ujangili.
Katika hatua nyingine, Wakazi wa
eneo hilo mara baada ya mkutano kuisha ,
walitoa zawadi ya gunia la mahindi pamoja na mbuzi ikiwa ni ishara ya kuonesha kufurahishwa na uamuzi wa kutembelea kijiji hicho kwa vile tangu kuanzishwa
kwake hakuna kiongozi yeyote mkubwa
aliyewahi kukanyaga katika hata hivyo baada ya kukabidhiwa zawadhi hzo naye
alitoa zawadi kwa shule ya msingi ya Ndondo ili wanafunzi waweze kula wakienda
shule.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Japhet
Hasunga (katikati), akioneshwa eneo la Pori Akiba la Lipalamba kutoka kwa Meneja
wa Pla akiba la Lipalamba, Ramadhan Isomanga wakati alipotenbelea Pori hilo
lililopo wilayani Nyasa mkoani Ruvuma ikiwa muendelezo wa ziara zake za kikazi
za kukabiliana na changamoto za uhifadhi maliasili, malikale na Uendelezaji Utalii.
No comments:
Post a Comment