Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son (wa pili kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda (kushoto), wakikata keki wakati wa uzinduzi wa huduma ya kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa. Wengini ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan
Long (kulia) na Meneja Biashara wa
Halopesa, Magesa Wandwi (wa pili kulia). Hafla hiyo ilifanyika Julai 3, 2018 jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan
Long, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo.Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Halotel, Mhina Semwenda, akizungumza katika uzinduzi wa huduma ya kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halotel Van Nguyen Son pamoja na Mkuu
wa Kitengo cha Mawasiliano wa Kampuni hiyo,Mhina Semwenda pamoja wa
wafanyakazi wengine wa Halotel wakigonga glass za shampeni kuashiria
uzinduzi wa huduma ya wateja wa Halopesa itakao wawezesha
kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa, wanaoshuhudia ni Mkuu wa
kitengo cah Halopesa Vu Tuan Longa (kulia) na Meneja biashara wa
Halopesa Magesa Wandwi (kushoto).
Kuondolewa kwa makato hayo inatafsiriwa
na kampuni hiyo kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa
mamilioni ya Watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa, Vu Tuan
Long, amesema kuwa kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao
huo hasa walioko katika maeneo ya vijijini kuweza kufanya miamala ya simu na
kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kuepuka kwa kutumia njia nyingine kutuma
fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.
“Tuna mamilioni ya watanzania ambao kwa mara
ya kwanza walipata mawasiliano ya simu tulipoanzisha huduma zetu, na baada ya
kuanzishwa kwa huduma ya Halopesa kwa miaka miwili sasa wateja wetu katika
maeneo mbalimbali wanaweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa,” Alisema
Long na kuongeza.
“Hii ni hatua nyingine ya kuhakikisha kwamba
wateja wanakuwa na wigo mkubwa wa kuweza kukidhi mahitaji yao katika nyanja
mbalimbali za kiuchumi, na kijamii kupitia huduma ya kifedha ya mtandao kwa ubora, ukaribu, uhakika na
usalama zaidi na kuepuka kwenda umbali mrefu kwaajili ya kufuata huduma za kifedha
kupitia benki”. Aliongeza Long.
Aidha Mkurugenzi huyo, alibainisha kuwa, licha
ya kuondoa gharama katika kutuma fedha, huduma ya kutuma fedha kutoka Halopesa
kwenda mitandao mingine imepunguzwa gharama ili iwe rahisi zaidi kwa wateja
wanaotuma pesa kwenda mitandao mingine ya simu pia waweze kutuma pesa kwa
gharama nafuu.
“Habari njema tuliyonayo kwa wateja wetu ni
kuwezeshwa kwa huduma ya Halopesa kuweza kutuma pesa kwenda mitandao yote, sasa
wateja wetu wataweza kutuma pesa kwenda mitandao mingine kwa gharama nafuu
zaidi kabisa,” alisema Long.
Tangu kuanzishwa kwa huduma ya
Halopesa tayari Mawakala Zaidi ya elfu 55,000 tayari wamejisajili na wanatoa
huduma kwa zaidi ya wateja milioni moja na nusu walioenea nchi nzima.
No comments:
Post a Comment