Lowassa akihutubia umati wa wananchi kwenye viwanja vya National Housing Kata ya Mto wa Mbu wakati wa uzinduzi wa kampeni za Ubunge Jimbo la Monduli.
Na Mwandishi Wetu
Waziri Mkuu mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa, amempongeza Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, kuwazuia wakuu wa mikoa na wilaya kuwaweka watu ndani hovyo.
Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za ubunge jimbo la monduli kwa tiketi ya chadema kwenye viwanja vya National Housing kata ya Mto wa Mbu, Lowassa amesema nchi ni lazima iongozwe kwa kuheshimu utawala wa sheria.

"Napenda kumpongeza Mh. Kangi Lugola waziri wa mambo ya ndani kwa kukemea kamata kamata iliyokuwa ikiendeshwa na wakuu wa mikoa na wilaya.
Ni lazima nchi iendeshwe kwa kuheshimu utawala wa sheria" alisema Lowassa ambaye anaongoza kampeni hizo ametilia shaka matokeo ya chaguzi zote za marudio akisema upinzani umekuwa ukifanyiwa hila.
"Nimekuwa najiuliza je ni kweli by election zote tunashindwa? Hapana kwa umati huu mliomfika mmeonesha kuwa upinzani bado una mvuto mkubwa sana katika jamii ya watanzania" alisema huku akishangikiwa na kuongeza Chadema wana uhakikaa mgombea wao atashinda.
Amepuuza kauli za mbunge aliyejiuzulu Kalanga kuwa Monduli hakuna maendeleo.

No comments:
Post a Comment