HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 29, 2018

MAZISHI YA MAMA YAKE SUGU KATIKA PICHA

Waombolezaji wakiusindikiza kuelekea kanisani mwili wa Mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi 'Sugu'.
Waombolezaji wakielekea kanisani.
Mwenyekiti wa Chadema, Freman Mbowe, akitoa salamu za rambirambi wakati wa ibada ya kuaga mwili.
Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye, Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema pamoja na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi wakielekea kanisani.
Wanafamilia pamoja na waombolezaji wakiwa kanisani. 

NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MWENYEKITI wa Chama cha Demkrasia na Meandeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema kuwa kama taifa hakutakuwepo na ushirikiano katika masuala ya uongozi, Siasa na masuala mengine ya kawaida katika jamii utakuwa ni unafiki kuonyesha kuwa kuna ushirikiano kwenye msiba.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana ndani ya Kanisa Kotoriji Parokia ya Roho Mtatifu Ruanda jimbo la Mbeya Mjini wakati wa ibada ya kuuga mwili wa mama mzazi wa Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi “Sugu’ Desideria Mbilinyi alifariki Jumapili katika Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Mbunge wa Vitia maalumi kupitia CCM Mkoa wa Mbeya Mary Mwanjelwa, Tumain Mwakatika, akitoa salamu alisema kuwa sauala na Msiba halina itikadi ndiyo maana hata wafuasi wa CCM wameshiriki.
‘Nimesimama hapa mbele kwa niaba ya Dk. Mwanjelwa ndugu zangu masuala ya msiba hayana itikadi ndiyo tumeungana na mwenzetu Sugu katika kipindi hiki kigumu’ alisema Tumaini.
Naye katibu wa Itikadi na ueneza CCM Mkoa wa Mbeya Bashiru Madodi alisema mama wa Sugu ni mama wa wana Mbeya wote.
‘Mama yako sugu ni mama yetu sisi siasa zifanyika kwenye majukwaa lakini siyo kwenye misiba ni yetu sote’ alisema Madodi.
Katika Msiba huo amabo ulihudhuria na zaidi ya wabunge 20 wa Chadema kauli hiyo ilimuinua Mbowe na kuomba nafasi ya kuongea  huku akieleza kuwa kama jamii wasipo shirikiana kwenye masuala yote kuonyesha ushirikiano kwenye msiba utakuwa ni unafiki.
‘Kama hatuwezi kushirikiana kwenye uongozi, siasa, kijamii au mambo ya kawaida utakuwa ni unafiki kuonyesha ushirikiano kwenye msiba’ alisema Mbowe.
‘Nakushukuru Mkuu wa Wilaya umezungumza ukweli lakini RC anabeza uwepo wa chama chetu Mbeya naomba umfikishie salamu lakini najua wazi kuwa chadema ipo na itaendelea kuwepo aliongeza.
Hata hivyo akiwa nyumbani kwa kina Sugu Mbowe alisema kuwa chama hicho kinapitia katika kipindi kigumu na siyo wakati wa kuteteleka bali na kuendelea kuwa imara zaidi.
‘Tunapita kipindi kigumu sana Chadema maana tunanyimwa kufanya mikutano sasa hili ndilo eneo pekee la kuzungumzia siasa japo tunapita kipindi kigumu lakini ndiyo wakati pekee wa kujiimarisha’ alisema Mbowe.
Alisema kipindi hiki ni wakati pekee wa kuonyesha umoja wao kama chama na wote wenye kupenda haki na wataungana na Chadema lakini wenye roho nyepesi wanakimbia.
Mbowe alisema kuwa kama si udhalimu wa viongozi walio madarakani huenda mama Sugu pengine mama huyo asingefariki kwani maradhi yake yametokea wiki moja tu tangu Sugu ahukumiwe gerezani kwa kosa la kutoa lugha za fedhea dhidi ya Rais John Pombe Magufuri.
Mbowe alisema safari ya uhai wa chama hicho inaza mwaka 2020 na kama wapo watu wanaosema ndo mwisho wa chama hicho wanajidanganya.
‘Safari ya chadema inaanza 2020 kama wapo watu wanasema ndo mwisho wa chadema wanajidanganya mwaka huo ndio itakuwa inaanza’ alisema Mbowe.
Akizungumza katika Msiba huo Waziri Mkuu mstaafu katika Serikali ya Awamu ya tatu Fredrick Sumaye, alisema kuwa anashanga kinachotokea Mbeya hasa kwa kuona msiba huo wapo pia viongozi wa Chama cha Mapinduzi CCM huku akieleza kuwa ni mfano wa kuigwa na maeneo mengine.
Nafarijika sana kuona msiba unavyo enda, CCM, Serikali, wapo nasema hili namanishga kwani hivi sasa kuna katabia kwenye tatizo na upande mwingine ni nadra kuona watu wa upande mwingine’ alisema Sumaye
Sumaye alisema kuwa Siasa ni utaratibu wa maisha ya binadamu na watu wanaweza kupingana katika majukwaa.
Mimi niwaomba yale ya kisiasa tuyaache kwani yatatupeleka pabaya Mbeya mmeonyesha mfano” aliongeza Sumaye
Akisoma wasifu wa mama yake Mbunge Sugu alisema kuwa mama yake alikuwa anasumbuliwa la B.P lakini chanjo kikubwa kilicho mpelekea mpaka mauti ni baada ya yeye kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano katika gereza la Ruanda Mkoa Mbeya.
‘Wiki moja bada ya mimi kufungwa kwa kuonewa ndipo mwanzo wa mama kuanza kuuamwa kwani hata yeye aliamini nimekwenda gerezani kwa kuonewa’ alisema Sugu.

No comments:

Post a Comment

Pages