Naibu
Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na
wenyeulemavu,Stella Ikupa akitamburishwa baadhi ya viongozi walioshiriki mkutano mkuu wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Naibu
Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na
wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwasili katika ukumbi wa J.K Nyerere uliopo Chuo Kikuu cha Ushirika,Moshi (MOCu) kwa ajili ya kufungua mkutano wa Tano wa chama hicho.
Naibu
Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na
wenyeulemavu,Stella Ikupa akizungumza wakati wa kufungua mkutano wa tano wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) unaofanyika mjini Moshi.
Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) Dkt Paul Loisulie akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania(THTU),Salma Fundi akizungumza katika mkutano huo.
Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Kippi Warioba akizungumza katika mkutano huo.
Mwakilishi wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu ca Ushirika Moshi (MOCU) Dkt Gudluck Mmari akizungumza wakati wa ufunguzi wa mkutano huo.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu Tanzania (THTU) Amina Mdidi akizungumza katika mkutano huo.
Mjumbe wa kamati ya wananwake ya THTU,Sophia Nchimbi akitoa neon la shukrani katika mkutano huo.
Naibu
Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na
wenyeulemavu,Stella Ikupa akiwa katika picha ya pmaoja na washiriki wa mkutano huo.
Na Dixon Busagaga, Moshi
CHAMA cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu Tanzania
(THTU) kimeiomba serikali kutunga sera ya uwepo wa eneo rafiki la kulelea au
kunyonyeshea watoto katika sehemu za Kazi
pamoja na kuunda chombo cha kusimamia utekelezwaji wa uwepo wa sera ya
unaynyasaji wa kijinsia katika taaasisi za elimu ya juu nchini.
Mbali na ombi hilo THTU pia kimewasilisha ombo kwa serikali
la kuundwa Vyombo vya kufuatilia waajiri ambao hawazingatii maagizo ya sera
zinazotungwa na serikali ili kulinda haki na maslahi ya wafanyakazi sambamba na uwepo wa muundo wa utumishi kwa
wafanyakazi waendeshaji katika taasisi za umma za elimu ya juu nchini.
Hayo yalibainishwa wakati wa mkutano mkuu wa tano wa chama hicho
unaofanyika kwa siku mbili katika Chuo Kikuu cha Ushirika ,Moshi (MoCU)
ukishirikisha zaidi ya wanawake 80 kutoka vyuo vikuu 36,vitatu vikiwa ni vya
binafsi na 33 vya serikali .
Katika risala yao kwa mgeni rasmi ,iliyosomwa na katibu wa
THTU,Amina Mdidi ,wanawake hao walisema THTU imekuwa ikikabiliwa na changamoto
nyingi ikiwemo ya kutokuwepo kwa mwongozo wa mishahara au bodi ya kusimamamia
na kudhibiti malipo ya watumishi kwa vyuo binafsi.
“Changamoto nyingine zinazootukabili ni baadhi ya taasisi
kutolipa nauli za likizo kwa enza wa wafanyakazi wanawake (Mume) na watoto
chini ya miaka mitano na ukosefu wa vituo rafiki kwa malezi ya watoto wachanga”alisema
Mdidi.
Katika hatua nyingine, Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za
Elimu ya Juu Tanzania kilitoa ripoti ya utafiti juu ya utekelezaji wa sera ya
maendeleo ya mwananmke na jinsia ya mwaka 2000 katika taasisi za elimu ya juu
Tanzania ikionyesha aslimia 80 ya taasisi hizo zilionyesha kutokuwepo kwa
masuala ya jinsia katika mpango mkakati wa taasisi.
Akisooma utafiti huo ,Mwenyekiti wa kamati ya Wanawake
(THTU) taifa Salma Fundi alisema asilimia 80 ya taasisi hazikuonyesha uwepo wa
mafunzo kwa wanafunzi au wafanyakazi kuhusiana na masuala ya jinsia.
“Asilimia 70 ya taasisi hazina sera ya unyanyasaji wa
kijinsia ambazo ni muhimu katika kupunguza ubaguzi wa kijinsia na ukatili huku
asiliamia 60 ya washiriki walikuwa na mtazamo hasi juu ya sera ya jinsia kwa
kuamini ni sera inayomhusu mwanamke tu”alisema Fundi.
Katika hotuba yake Mgeni rasmi katika ufunguzi wa mkutano
huo,Naibu Waziri ,Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,kazi ,Vijana,Ajira na
wenyeulemavu,Stella Ikupa alisema THTU
kwa muda mfupi kimekuwa chama kinachotoa chachu ya maendeleo na amani ndani ya
taasisi za elimu ya juu Tanzania.
“Ni chama ambacho kiko makini katika shughuli zake za
utatuzi na hata mfumo na uwasilishaji wa hoja zake umekuwa ni wa aina ya
kipekee kwa kufanya tafiti zilizochambuliwa kwa kina wa nini wanawake
wanafikilia kifanyike”alisema Ikupa.
Waziri Ikupa aliyekuwa akimuwakilisha Waziri wan chi ,ofisi
ya Waziri Mkuu Sera ,Bunge,KAZI,Vijana ,Ajira na Wenyeulemavu ,Jenista Mhagama aliahidi
kuwasilisha mapendekezo yao pamoja na changamoto walizo wasilisha kwa serikali
kwa ajili ya kuafanyiwa kazi.
No comments:
Post a Comment