Waziri Mkuu, Kassim
Majaliwa akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Singida, Paskasi Mragili
wakati aliposimama kwa muda mfupi miini Singida alipokuwa njiani kwenda
Igunga mkoani Tabora kwa ziara ya kazi Agosti 16, 2018. Mragili alikuwa
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu hadi Mamlaka hiyo
ilipovunjwa. Katikati ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majaliwa. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu).
WAZIRI
MKUU Kassim Majaliwa amemuagiza Kamanda wa TAKUKURU wa wilaya ya Igunga
mkoani Tabora, Bw. Francis Zuakuu kumkamata aliyekuwa Mtendaji wa
Kijiji cha Bulagamilwa, Bw. Ntemi James kwa tuhuma za kuhusika na
upotevu wa sh. milioni 141 za kijiji hicho.
Ametoa
agizo hilo leo (Alhamisi, Agosti 16, 2018) wakati akizungumza na
watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Igunga, akiwa katika siku ya
kwanza ya ziara yake ya kikazi ya siku tatu mkoani Tabora.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo baada ya Mbunge wa Manonga, Bw. Seif Gulamali
kumuomba awasaidie katika kulipatia ufumbuzi suala hilo la upotevu wa
fedha za kijiji kwa kuwa ni la muda mrefu na hakuna hatua
zilizochukuliwa.
Kutokana
na malalamiko hayo Waziri Mkuu amemtaka kamanda wa TAKUKURU wa wilaya
hiyo ahakikishe anawatafuta watu wote waliohusika na upotevu wa fedha
hizo za kijiji akiwemo na alitekuwa mtendaji wa kijiji cha Bulagamilwa,
ambaye kwa sasa ni Mtendaji wa kata ya Igurubi.
Katika hatua nyingine,Waziri Mkuu amewataka watumishi wa umma wilayani Igunga wahakikishe wanatimiza wajibu wao ipasavyo kwa kuwatumikia wananchi kwa weledi na ustadi bila ya ubaguzi wa aina yoyote.
Waziri Mkuu amesema watumishi wa umma lazima wabadilike na wafanye kazi kwa bidii, waachemazoea na
watumie utalaamu wao vizuri katika kuwahudumia wananchi na Serikali
haitowavumilia wafanyakazi watakaoshindwa kutekeleza majukumu yao.
"Msimamo
wa Serikali ni kuhakikisha wananchi wanahudumiwa ipasavyo, hivyo
haitawavumilia watumishi whv atakao jihusisha navitendo vya rushwawa na
matumizi mbaya ya fedha za umma."
Pia
Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara na watumishi wengine wajiwekee
utaratibu wa kuwatembelea wananchi katika maeneo yao hususan ya vijijini
kwa ajili ya kusikiliza kero zinazowakabili na kushirikiana nao katika
kuzipatia ufumbuzi.
No comments:
Post a Comment