HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

August 01, 2018

RAIS WA ZANZIBAR DK.ALI MOHAMED SHEIN AWASILI NCHINI INDONESIA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati), akifuatana na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania nchini Indonesia, Dk. Ramadhani Dau, baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mwaliko wa Makamu wa Rais wa nchini Indonesia Mhe. Mohammed Jusuf Kalla.. (Picha na Ikulu).
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania Nchini Indonesia Mhe.Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) na Viongozi wengine wakipewa maelekezo na Afisa Maalum mara baada ya mapokezi walipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo wakiungana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) katika ziara ya siku saba Nchini humo kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akisalimiana na Kiongozi wa Ngazi ya Juu Nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (kushoto) mara alipowasili katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali, katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Malaysia pia akiwakilisha Tanzania nchini Indonesia Mhe. Dkt Ramadhani Kitwana Dau (kulia) mara alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta Indonesia leo, akifuatana na Mkewe Mama Mwanamwema Shein pamoja na Viongozi mbali mbali, katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchi hiyo Mhe.Mohammed Jusuf Kalla.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) pamoja na Viongozi aliofuatana nao akiwa katika mazungumzo na Kiongozi wa Ngazi ya Juu nchini Indonesia Daniel T.S.Simanjuntak (wa pili kulia) katika Ukumbi wa Watu Mashuhuri katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Soekarno Hatta, Jakarta katika ziara ya kikazi ya siku saba kwa mualiko wa Makamo wa Rais wa Nchini Indonesia Mhe.Mohammed Jusuf Kalla. (Picha na Ikulu).

No comments:

Post a Comment

Pages