Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi (kulia), akimkabidhi mfano wa hundi Mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Ibrahim Mbwilo (28) ambaye ameshindia Sh milioni 239.4. Mbwilo ni Mwanafunzi wa Mwaka wa Pili wa Chuo Kikuu Cha Iringa. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam. Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa, Ibrahim
Pius Mbwilo (28) ameshinda Sh 239,417,800 kupitia mchezo wa Perfect 12
unaoendeshwa na kampuni ya M-Bet.
Mbwilo ambaye anasoma shahada ya Utawala wa Biashara
(Business Administration) akiwa mwaka wa pili, alibashiri kiusahihi mechi 12 za
ligi mbalimbali za ulaya.
Meneja Masoko wa Kampuni ya M-Bet, Allen Mushi alisema kuwa
Mbwilo ambaye ni shabiki wa timu ya Simba na Chelsea ya Uingereza, amekuwa
mshindi wa pili kupata fedha nyingi zaidi tokea kuanzishwa kwa droo ya Perfect
12. Mshindi wa kwanza alipata Sh 280 millioni.
Mushi alisema kuwa M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa
na kuwasaidia watanzania kubadili maisha yao kwa kutumia Sh1,000 tu.
“Nawaomba Watanzania kuendelea kubashiri kwa kutumia michezo
yetu,kuna nafasi kubwa ya kushinda na mpaka sasa tumepata jumla ya washindi 10
ambao wamefaidika na droo yao,” alisema Mushi.
Alisema kuwa Serikali imepata Sh 47 millioni kutokana na
kodi kutokana na ushindi huo wa Mbwilo.
Akizungumza baada ya
kupokea hundi yake, Mbwilo alisema kuwa amefarijika sana kupata fedha hizo ambazo
atazitumia kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo, kuwasomesha ndugu zake na
kusaidia familia.
Mbwilo alisema kuwa pia atatumia fedha hizo kwa ajili ya
kuendeleza biashara yake ya kuuza matofali na kuanzisha biashara nyingine.
Alisema kuwa yeye ni mtoto yatima na aliishi maisha ya
mitaani huku akiokota taka na kuziuza kama mbolea (samadi) kwa akina mama ambao
walikuwa wateja wake kwa lengo la kumsaidia.
“Niliishi mitaani,
nilikwenda jalalani kutafuta matunda, taka, kutafuta taka na kuziuka kama mbolea,
nilifanya hivyo baada ya kuachwa na mlezi wangu nikiwa kidato cha pili, naguswa
na aina hiyo ya watoto yatima hiyo.
“Tarehe 6 mwezi huu, nilitumia sh 1,000 kubashiri na kupata
kiasi kikubwa cha fedha, namshukuru Mungu kwani wanaobashiri wengi, nitasaidia
kituo cha watoto yatima kwa kunua magodoro, kuna kituo cha watoto yatima ambao
hawana vitanda hata magodoro, nitafanya hivyo kwa sababu mimi mwenyewe
nimetokea huko,” alisema Mbwilo.
No comments:
Post a Comment